Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu waTanzania Mhe Mohamed Chande Othman pamoja na ujumbe wake walipomtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.  

Jaji Mkuu na ujumbe wake wako Marekani kwa ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine yeye na ujumbe wake watahudhuria mkutano maalumu wa kimataifa wa Mabadiliko ya Sheria ya Ushahidi jijini Washington  na pia kukutana na taasisi mbalimbali za fedha na marafiki wa maendeleo katika ili  kupata wabia wa ujenzi wa maendeleo ya mahakama. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula, Jaji wa Mahakama ya rufani Mhe Ibrahim Juma, Msajili wa Mahakama Kuu Mhe Ignass Kitusi,daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi na Mtendaji Mkuu wa Mahakama
Mhe Hussein Katanga.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman aliyemtembelea na kumjulia hali Jumapili Novemba 16, 2014 katika hoteli maalumu jirani na Hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore, Maryland, Marekani anakoishi baada kutoka katika hospitali hiyo alikofanyiwa upasuaji wa tezi dume.
 Rais Kikwete akiongea na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa twakupa pole.
    Michuzi bila shaka kuna student doctors na wengine wanaopenda kujua kwa nini raisi aonekana hapo kavaa stocking nyeupe.Jibu ni kwamba baada ya operashen ya tezidume kuna hatari kubwa ya damu kufanya mgando kwenye miguu, wataalam waita DVT ua deep vein thrombosis, na baadaye kupata ile kitu kiitwacho PET yaani pulmonary thrombosis, ambayo yaua.Hizo soks na shindano za heparin ni katika kuzuia matatizo hayo. Allah yebarik

    ReplyDelete
  2. Mh. Rais We Wish You A Speedy Recovery.

    Mdau wa kwanza hapo juu ameongelea jambo la kutiliwa maanani, maana mara nyingine safari ndefu ktk presurrised cabin ya ndege pia huweza kusababisha DVT - Deep Vein Thrombosis.

    Inabidi mkulu pia apunguze safari za ndege za masafa marefu ktk schedule zake, na DVT inaweza kumpata mtu yeyote akaaye chini kwa muda mrefu ndani ya ndege.


    ReplyDelete
  3. Anonymous hapo umefanya la maana kuelezea hiizo stockings kabla jamaa hawajaanza kuosha vinywa..maana hilo tuko mstali wa mbele..tunamtakia mheshimiwa azidi kupata nafuu na kuruhusiwa ili kuendelea kukabli majukumu ya nchi.
    UGUA POLE.

    ReplyDelete
  4. Ann hapo juu well said. Hiyo ni DVT prophylaxis kwa kuvaa Ted stockings.

    ReplyDelete
  5. Nakuombea sana kwa Mwenyezi Mungu Rais wetu mpendwa upone haraka na urudi nyumbani salama ili uendelee na majukumu ya kuongoza Taifa letu. Ugua pole Mheshimiwa Rais. Mdau wa libeneke, Sweden.

    ReplyDelete
  6. Pole sana Mhe. Rais wetu. Mdau wa kwanza katufungua macho sisi laymen kuhusu mambo ya kitabibu. Ahsante sana Mdau. Ugua pole sana Mhe. Rais wetu, mimi sikufikiria ukubwa wa ugonjwa uliokuwa nao, nilidhani ni uchunguzi na kurekebishwa maradhi ya kawaida madogo madogo, lakini jinsi nilivyokuona baada ya upasuaji nikapata jibu kamili, pole sana Kiongozi wetu shujaa na mwenye upendo mkubwa kwetu Watanzaniana Tanzania yetu yote. Hakunaga mwingine...labda baada yako tutapata, kwa sasa hakunaga.

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...