
“Nimehuzunishwa
na kusikitishwa na taarifa za kifo cha Mwanamuziki
Khamisi
Kayumbu kilichotokea tarehe 9 Novemba, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo”, amesema
Rais Kikwete katika Salamu zake.
Rais Kikwete amesema anatambua mchango mkubwa wa
Marehemu Amigolas, katika kuhamasisha maendeleo ya nchi yetu, kupitia sanaa ya muziki
katika kuwafikishia wananchi ujumbe muhimu wa masuala mbalimbali ya kijamii na
kiuchumi. Amesema kuwa Hayati Kayumbu alikuwa mfano unaofaa kuigwa na Wasanii wengine kote nchini.
“Kutokana
na msiba huu, naomba upokee Salamu zangu za Rambirambi kwa kumpoteza mmoja wa
Wanamuziki Mahiri hapa nchini, na Rambirambi hizi ziwafikie pia Wanamuziki
wengine kote nchini kwa kumpoteza mwenzao”.
Aidha,
Rais Kikwete amemwomba Dkt. Fenella Mukangara kumfikishia Salamu zake za Pole
kwa Familia ya Marehemu Khamisi Kayumbu kwa kupotelewa na Kiongozi na Mhimili
madhubuti wa Familia.
Mwisho.
Imetolewa
na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
10 Novemba,2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...