Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Miundombinu wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata (km 64), inayojengwa kwa kiwango cha lami. Barabara hii inaunganika na barabara kuu ya Dar es salaa – Chalinze – Arusha katika eneo la Msata. Hivyo ni njia mbadala ya kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kanda ya Kaskazini na nchi jirani ya Kenya.

Barabara hii inayojengwa na kampuni ya Estim Construction ltd, na kusimamiwa na mhandisi mshauri kampuni ya JBG Gauff Ingenieure GMBH & Co. Mkandarasi wa barabara hii ya Bagamoyo – Makofia – Msata anatarajia kukabidhi barabara hii Machi, 2016.

Aidha, kamati hiyo ilipata nafasi ya kutembelea mizani ya kisasa iliyopo eneo la Vigwaza inayojengwa na kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) na mhandisi mshauri kampuni ya Ambicon Engineering Ltd of Tanzania. 

Mradi huu hadi sasa umekamilika kwa asilimia 95. Ikiwa ni kukamilika kwa barabara ya maingilio, maegesho ya magari, majengo, ofisi, gereji na jenereta, vyoo vya wasafiri pamoja na mizani. 

Mradi huu unakamilika Novemba 2014. Kwa habari zaidi tazama picha za ziara hiyo.(Imetolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini – Wizara ya Ujenzi)
Naibu waziri wa Ujenzi Mhe. Gerson Lwenge (Mb) akiwasili eneo la mradi akiambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba.
Wajumbe wa kamati ya bunge ya Miundombinu wakipata taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya lami Bagamoyo – Makofia – Msata (Km 64) kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale.
Ramani ya mchoro ambao barabara ya Bagamoyo – Makofia – Msata itaungana na barabara ya Dar es salaam – Bagamoyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...