Kutoka kushoto ni: Lwitiko Mwakilasa, Bernard Kakengi, Mapinduzi Mwankemwa, Mzee Kimaro wa JWTZ, Victor Gunze wa TBC, Raymond Mutafungwa. Rupia Lyabandi, Dennis Londo, Ankal Muhidin Issa Michuzi, Fidelis Tungaraza "Mti Mkubwa", Ndesanjo Macha, Magonera Malima na Kisakisa Kiwala.
Taswira hii ni ya Septemba 10, 2005 katika kiota cha maraha kinachopendwa sana na Wabongo cha Chelsea hapo jijini Helsinki Finland. Tukio ni mkusanyiko wa wadau kusherehekea kuanzishwa rasmi kwa Globu ya Jamii takriban miaka 10 iliyopita. Hii ilikuwa ni pembeni mwa mkutano wa Helsinki (Helsinki Conference) ambao Rais Benjamin Mkapa (wakati huo) alihutubia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania (wakati huo) Mhe Jakaya Mrisho Kikwete na mwenzake wa Finland, Mhe Errik Tuomioja, walikuwepo, pampja na Dkt Asha-Rose Migiro (wakati huo akiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto)
Ni kweli kwamba Ndesanjo Macha (aliyesimama kulia na gwanda la bluu) ndiye aliyefanikisha kuanzishwa kwa Libeneke hili pale jirani na hapo Chelsea, katika ukumbi wa Finlandia, si uwongo kwamba Fide Tugaraza (kifuani pa Ankal, na kulia kwa Ndesanjo, ndiye aliyesababisha yote haya kutokea kwa msimamo wake wa kumcharura Ankal na wanahabari wa Bongo, kwamba kwa nini hawaleti vitu vya nyumbani mtandaoni?
Yaani kama si yeye (Fide) Globu ya Jamii isingekuwa hai hii leo. Na Kama si Ndesanjo kumpa lekcha Ankal ya nanmna ya kuanzisha blogu, tungekuwa tunaongea nini sijui saa hizi.
Yaani kama si yeye (Fide) Globu ya Jamii isingekuwa hai hii leo. Na Kama si Ndesanjo kumpa lekcha Ankal ya nanmna ya kuanzisha blogu, tungekuwa tunaongea nini sijui saa hizi.
Kwa heshima na taadhima Globu ya Jamii inapenda kutoa saluti kwa mkusanyiko huu wa kihistoria ambao mbali na kuwa wadau wa mwanzo wa Libeneke hili, pia wadau hawa ndio waliosimama kidete kuhakikisha hakuna kinachoharibika. ASANTENI SANA SANA FIDE NA NDESANJO pamoja na wadau wote katika taswira hii ya kihistoria. Hatuna cha kuwalipa zaidi ya kusema AHSANTENI AHSANTENI SANA SANA.
priceless moments!
ReplyDeleteEh Ankal leo umeamua kutoa yaliyo moyoni kabisa!
ReplyDeleteNi funzo zuri sana kuwashukuru wale waliokusaidia kufanikisha malengo yako.
Tunakupa hongera sana
Ankal, jana nimeifukua mahali hii picha, nikakumbuka mbali sana, Mungu akujalie na kukuongezea Palipopungua kamanda-Mapinduzi Mwankemwa hapa aka Mapi
ReplyDeleteHongereni sana sana! Long live Michuzi Blog...
ReplyDeleteYes Sir,
ReplyDeleteBlog hii inabaki kuwa na sifa kadhaa za pekee:
1: Ni blog ya ambayo imekuwa active katika kipindi cha takriban miaka kumi sasa. Imekuwa ikihabarisha kila siku bila kupoteza hata siku moja tangu siku ilipoanzishwa hadi leo.
2: Ni Blog ambayo imekuwa inahabarisha mambo mbali mbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Pia umekuwa ni ukumbi wa huru wa watu mbali mbali kuleta mijadala ya kijamii, kisiasa na kiuchumi na habari binafsi mathalani za kuzaliwa, misiba, harusi, mahafali, kupotelewa na watoto, ndugu, jamaa, marafiki na vitu binafsi kama vyeti, nyaraka, mikoba na vitu vingine, kadhalika kutafutana kwa ndugu, jamaa na marafiki. Matangazo ya kazi na masomo.
3: Ni Blog ambayo inasomwa na kupitiwa na wengi ndani na nje ya Tanzania.
4: Ni Blog inayotegemewa na wengi katika kutoa habari mpya (Breaking news) za mambo mbali mbali ya Tanzania.
Ongezea wewe mwenzangu
5:
6:
7:
Na kuendelea
Mkuu Michuzi Hongera sana.
Ni mimi maridhiya,
F MtiMkubwa Tungaraza, Helsinki, Finland.