Makamu wa Rais wa Kiwanda cha Dawa za
Binaadamu cha Shuangcheng Bwana Jianlin Yuan akimpatia
maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na
Ujumbe wake wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiwa
katika ziara ya Kiserikali Katika Jimbo la Kisiwa cha
Hainan.
Ujumbe wa Zanzibar Ukiongozwa na Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif ukifanya mazungumzo
na Ujumbe wa Makampuni ya uwekezaji vitega uchumi katika
Jimbo la Hainan ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara
ya Nyumba na Maendeleo ya Miji na Vijiji ya Hainan.
Balozi Seif na Ujumbe wake wakiwa katika
kikao cha pamoja cha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uongozi
wa Manispaa ya Mji wa Haikou ukiongozwa na Meya wa Mji
Huo Mstahiki NI Qiang.
Mwenyekiti wa Kiwanda cha kusindika bidhaa
za nazi pamoja na matunda kiliopo Haikuu Bwana Huang
Chunguang akimfahamisha Balozi Seif na Ujumbe juhudi
zinazochukuliwa na Kiwanda hicho katika kulitumia vyema zao
la nazi.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi na
Kulia yake ni Waziri wa Ardhi Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban
na Waziri wa Habari Mh. Sai Ali Mbarouk.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...