Habari wadau, kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.  Pia mwandishi mahiri wa zamani wa habari za michezo nchini Innocent Munyuku, naye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Hilo ni pigo kwa waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla, maana wote wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana. Taarifa zaidi tutaendelea kupeana kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
19/11/2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hii ni Balaa , How can this Happen ? Ewe Mwenyezi Mungu tunusuru Waja wako . Poleni wafiwa , familia , marafiki , ndugu wa karibu , na wana Tasnia wote wa Habari , hususan za mchezo ! Alilo amua Mwenyezi Mungu , hatuna la kukosoa ! R.I.P. great souls of the nation
    - tonny

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...