Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Forum
CC imeandaa kongamano la siku moja kwa vijana kutoka Asasi za kiraia lililojadili msimamo wa
Tanzania juu ya masuala ya Mazingira, hususan Mabadiliko ya Tabianchi kuelekea Mkutano Mkubwa wa Mazingira Duniani
utakaofanyika katika jiji la Lima nchini Peru, Desemba 2014.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kufungua
kongamano hilo.
Sehemu ya Washiriki walioshiriki
katika kongamono hilo la siku moja lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya
kiserikali ya Forum CC wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akijibu maswali ya washiriki katika kongamano
la vijana jijini Dar es Salaam katika Hotel ya JB Belmont. Kongamano hilo la
siku moja lililenga kukusanya maoni ya vijana na kuainisha changamoto katika
suala zima la Hifadhi ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi.
Naibu
Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu (wa kwanza kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo. Wengine katika
picha, (waliokaa) ni Bi. Grace Munna, Mkurugenzi wa Program kutoka Forum CC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...