Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani. 
 Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo. 
 Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. 
Hali ya Mheshimiwa Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba. 
 Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana. 
 Imetolewa na
 KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,
 IKULU DAR ES SALAAM, NOVEMBA 9, 2014
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na  Dkt.Edward Shaeffer wa  hospitali ya Johns Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi  (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland nchini Marekani Jumamosi asubuhi(picha na Freddy Maro)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Pole utapona haraka

    ReplyDelete
  2. Pole sana Rais wetu mpendwa, Mola atakuafu upate nafuu ya haraka.

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kutujuza hali ya Kiongozi wetu.. Mungu akujalie afya njema kwa haraka mhesimiwa Rais

    ReplyDelete
  4. BWANA akutangulie Rais wetu mpendwa ...
    Tango Mike - Arusha

    ReplyDelete
  5. Mwenyezi Mungu akujalie upone haraka. Amin

    ReplyDelete
  6. m/mungu akujalie afya njema na uponyaji wa haraka

    ReplyDelete
  7. Raha ya kuwa wazi na mkweli ndio hii sasa. Alipoondoka mlitupa taarifa na picha juu kwamba anaenda kufanyiwa uchunguzi wa afya, na kuwa amegundulika ana matatizo na upasuaji umefanywa salama bin salimini. Haya ndio mambo tunataka maana mkiacha hivi hivi hawakawii kuzusha ya kuzusha mitandaoni. Sasa tunasubiria maendeleo yake kila siku. Tunampenda raisi wetu ati!

    ReplyDelete
  8. Kila lakheri Kiongozi wetu mpendwa JK.

    ReplyDelete
  9. GET WELL SOONEST MR PREZ

    - UR FANS IN THE UK

    ReplyDelete
  10. HIYO NI PROSTATE, NA SIO PROSTRATE ULIVYOSEMA...
    POLE MR PRESIDENT

    ReplyDelete

  11. POLE MR PRESd, kwa sasa Mr Pres anahitaji muda wa kujiangalia na kupumzika vzr kwani with prostate surgery, high likely hormone treatment will follow and radiation therapy at later stage...

    ReplyDelete
  12. MHE.RAIS WETU DKT. JK TUNAKUOMBEA AFYA NJEMA MWENYEZI MUNGU AKUFANYIE WEPESI KATIKA TIBA UPONE KWA HARAKA,INSHALLAH
    MUNGU AKUPE AFYA NJEMA
    Wadau
    Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mungu akujaalie afya njema baba yetu mpendwa.

      Delete
  13. Yaani hadi raha. Mgonjwa bado ana-smile tu hadi kitandani. BRAVO our Prezidaaa.
    We noma!

    ReplyDelete

  14. of course "wait and see policy" itakuwa poa baada ya surgery kabla ya ku rush for hormone trt au radiation therapy...get well soon mr Presdaa

    ReplyDelete
  15. Get well soon Mr.President.

    Ila kwanini Mr. Pres aende kutibiwa Marekani na si Muhimbili (hospital ya Taifa).Poor services hehe! Haya wee ndio nchi yetu. I never see People questioning this issue ya viongozi kutibiwa nje ya nchi. Kwani nani anatakiwa kuboresha huduma za hapa nchini.

    ReplyDelete
  16. God bless our dear presidaaa

    ReplyDelete
  17. Tunamuombe Mh. Rais apone haraka.. dua zetu watanzania ni muhimu

    ReplyDelete
  18. Get well soon our presdent

    ReplyDelete
  19. Where is the First Lady?!

    ReplyDelete

  20. mihimbili haiwezi kufanya upasuaji huu ? poor africans

    ReplyDelete
  21. Millions of Tanzanians do not get the same treatment. He needs to work hard in his final year to ensure that they do! Get well

    ReplyDelete
  22. is getting better and better and better

    ReplyDelete
  23. POLE SANA RAIS, SOTE TUPO NAWE KATIKA MAUMIVU, GET WELL SOON.

    ReplyDelete
  24. Pole sana Mheshimiwa Rais wetu JK. In Sha Allah Mwenyeez Mungu atakuafu na kukujaalia shifaa upone salama salimini na khatimae uweze kuendelea na shughulizo kama kawaida. In Sha Allah - Ameen.

    ReplyDelete
  25. Pole rais wa nchi yetu na Mungu atakupa wepesi ili urudi mapema kwa nchi yako

    ReplyDelete
  26. Mwenyezi Mungu akujalie afya njema Mheshimiwa Rais wetu upate kupona haraka.

    ReplyDelete
  27. mola akupe afya njema urudi nyumbani salama, na uende mafia kwa mpamziko ya wiki moja ni mahali pazuriiiiiiiiiiii kwa mapumziko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...