Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa
upasuaji wa tezi dume (prostate) katika Hospitali ya Johns Hopkins
iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia
uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji
matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Hali ya Mheshimiwa
Rais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini
ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.
Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete
kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.
Imetolewa na
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS,
IKULU
DAR ES SALAAM,
NOVEMBA 9, 2014
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Dkt.Edward Shaeffer wa hospitali ya Johns Hopkins (kushoto) na Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi (kulia) muda mfupi baada ya kuwasili ili kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland Marekani Jumamosi asubuhi.Upasuaji huo uliochukua muda wa saa moja na nusu ulifanyika salama.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na daktari Bingwa Mpasuaji Edward Shaeffer muda mfupi kabla ya kuingia kwenye chumba cha upasuaji uliofanyika katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland nchini Marekani Jumamosi asubuhi(picha na Freddy Maro)
Pole utapona haraka
ReplyDeletePole sana Rais wetu mpendwa, Mola atakuafu upate nafuu ya haraka.
ReplyDeleteAsante kwa kutujuza hali ya Kiongozi wetu.. Mungu akujalie afya njema kwa haraka mhesimiwa Rais
ReplyDeleteBWANA akutangulie Rais wetu mpendwa ...
ReplyDeleteTango Mike - Arusha
Mwenyezi Mungu akujalie upone haraka. Amin
ReplyDeletem/mungu akujalie afya njema na uponyaji wa haraka
ReplyDeleteRaha ya kuwa wazi na mkweli ndio hii sasa. Alipoondoka mlitupa taarifa na picha juu kwamba anaenda kufanyiwa uchunguzi wa afya, na kuwa amegundulika ana matatizo na upasuaji umefanywa salama bin salimini. Haya ndio mambo tunataka maana mkiacha hivi hivi hawakawii kuzusha ya kuzusha mitandaoni. Sasa tunasubiria maendeleo yake kila siku. Tunampenda raisi wetu ati!
ReplyDeleteKila lakheri Kiongozi wetu mpendwa JK.
ReplyDeleteGET WELL SOONEST MR PREZ
ReplyDelete- UR FANS IN THE UK
HIYO NI PROSTATE, NA SIO PROSTRATE ULIVYOSEMA...
ReplyDeletePOLE MR PRESIDENT
ReplyDeletePOLE MR PRESd, kwa sasa Mr Pres anahitaji muda wa kujiangalia na kupumzika vzr kwani with prostate surgery, high likely hormone treatment will follow and radiation therapy at later stage...
MHE.RAIS WETU DKT. JK TUNAKUOMBEA AFYA NJEMA MWENYEZI MUNGU AKUFANYIE WEPESI KATIKA TIBA UPONE KWA HARAKA,INSHALLAH
ReplyDeleteMUNGU AKUPE AFYA NJEMA
Wadau
Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni
Mungu akujaalie afya njema baba yetu mpendwa.
DeleteYaani hadi raha. Mgonjwa bado ana-smile tu hadi kitandani. BRAVO our Prezidaaa.
ReplyDeleteWe noma!
ReplyDeleteof course "wait and see policy" itakuwa poa baada ya surgery kabla ya ku rush for hormone trt au radiation therapy...get well soon mr Presdaa
Get well soon Mr.President.
ReplyDeleteIla kwanini Mr. Pres aende kutibiwa Marekani na si Muhimbili (hospital ya Taifa).Poor services hehe! Haya wee ndio nchi yetu. I never see People questioning this issue ya viongozi kutibiwa nje ya nchi. Kwani nani anatakiwa kuboresha huduma za hapa nchini.
God bless our dear presidaaa
ReplyDeleteTunamuombe Mh. Rais apone haraka.. dua zetu watanzania ni muhimu
ReplyDeleteGet well soon our presdent
ReplyDeleteWhere is the First Lady?!
ReplyDelete
ReplyDeletemihimbili haiwezi kufanya upasuaji huu ? poor africans
Millions of Tanzanians do not get the same treatment. He needs to work hard in his final year to ensure that they do! Get well
ReplyDeleteis getting better and better and better
ReplyDeletePOLE SANA RAIS, SOTE TUPO NAWE KATIKA MAUMIVU, GET WELL SOON.
ReplyDeletePole sana Mheshimiwa Rais wetu JK. In Sha Allah Mwenyeez Mungu atakuafu na kukujaalia shifaa upone salama salimini na khatimae uweze kuendelea na shughulizo kama kawaida. In Sha Allah - Ameen.
ReplyDeletePole rais wa nchi yetu na Mungu atakupa wepesi ili urudi mapema kwa nchi yako
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akujalie afya njema Mheshimiwa Rais wetu upate kupona haraka.
ReplyDeletemola akupe afya njema urudi nyumbani salama, na uende mafia kwa mpamziko ya wiki moja ni mahali pazuriiiiiiiiiiii kwa mapumziko
ReplyDelete