Hii ndio Barua iliyoandikwa na Miss Tanzania 2014,Sitti Mtevu kwenda kwa kampuni ya Lino International Agency ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo ya Urembo hapa nchini.
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) aliyechukua nafasi yake pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk.
Sitti Abas Mtemvu amelivua taji hilo baada ya kuiandikia barua Kamati ya Miss Tanzania, November 5 mwaka huu, kuhusiana na uamuzi wake huo.
Mrembo huyo alikuwa akikabiliwa na shutuma za kudanganya umri wake, jambo ambalo lilililazimu Baraza la Sanaa la Taifa, (Basata) kutokana na agizo la wizara  husika kufuatilia ukweli wake.
“Baada ya kutwaa taji la urembo la Miss Tanzania kumezuka shutuma mbalimbali dhidi yangu. Wameniwekea maneno mengi sana mdomoni kwamba nimesema wakati siyo,” amesema kwenye barua hiyo.
Miss Tanzania aliyechukua nafasi ya Sitti Mtemvu, Lilian Kamazima pichani kulia.
“Shutuma hizo zimeandikwa katika vyombo mbalimbali vya habari, blogs na mitandao ya kijamii, kiasi ambacho naweza hata kuhatarisha maisha yangu. Sasa kwa hiari yangu tena bila kushawishiwa na mtu na kwa kulinda heshima yangu na familia yangu natamka rasmi kuvua taji la urembo la Miss Tanzania 2014,” ameongeza.

“Napenda niwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa sapoti tangu mwanzo nilipoingia katika mashindano haya katika ngazi ya taifa, na warembo wote wa Chang’ombe, Temeke pamoja na wote tuliokuwa nao katika fainali za Taifa. Pia napenda kutuma shukrani za dhati kwa waandaji wote wa kituo cha Chang’ombe, Temeke na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania kwa mafunzo mbalimbali niliyopata. Nawashukuru pia waandishi wote kwa mchango wenu, pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na Baraza la Sanaa kwa busara zenu.”
Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Mtemvu katika pozi. 
“Leo nalivuta taji rasmi nililopewa na binadamu lakini alilonipa mwenyezi Mungu bado ninalo. Mwisho naomba radhi Watanzania wote kwa uamuzi huo niliochukua.” Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa mshindi wa pili, Lilian Kamazima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sour looser. Not even a word of congratulation to her successor!

    ReplyDelete
  2. Bado hajutii kudanganya kwake. Anaona watu tu wamemsakama bila sababu. Wabongo iko kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  3. Huyu wa sasa ndio ana umri gani? mi naona kama wale wale tu.

    ReplyDelete
  4. Hata kama kalivua hilo taji bado tunataka kujua kauli ya uchunguzi toka baraza la michezo na kama ni kweli alidanganya na arudishe taji la changombe-Temeke

    ReplyDelete
  5. Tehtehteh bado unamalizia na jeuri yenye kiburi dah rekebisha moyo wako hata kumpongeza mwenzako unaona watu wamekufanyia Choyo? Choyo umejifanyia mwenyewe na kuhusu kuvaliwa na watu na mungu amekupa bado unalo ni kweli ila kumbuka Mungu umeongopea wanadamu wake pia kwahiyo tubia kwa mungu na wacha tabia yako chafu ya roho.

    ReplyDelete
  6. Mazoea ya kuhalalisha haramu kuwa halali

    ReplyDelete
  7. Watanzania tubadilike...huyu binti yafaa awajibishwe kwa yote yaliyotokea. Huu pia ni aina ya UFISADI!!! Taasisi zilizohusika ikiwa ni pamoja na RITA na kamati ya mashindano ya bwana Lundenga pia nao wawajibike na ikishindikana basi wawajibishwe.

    ReplyDelete
  8. Bwana Lundenga wewe ni mwana Yanga mwenzangu, lkn kwa huu upuuzi unaofanya ktk tasinia hii ya urembo sitakuwa nawe. Inawezekanaje moja ya vielelezi muhimu (cheti cha kuzaliwa) ktk mashindano kipatikane siku chache
    kabla ya kufanyika?????? Vielelezi hivi yafaa viwasilishwe mapema pindi mashindano yanapoanza siyo kama alivyofanya huyo mrembo wako!

    ReplyDelete
  9. Vipi sasa kuhusu kuwa mcha Mungu? Kwani umekiri kuna taji kakupa! Ili iwe shukurani kutoka kwako.

    ReplyDelete
  10. Nilikuwa sifuatilii mjadala ila huyo namba mbili moto...

    ReplyDelete
  11. Inabidi arudishe zawadi alizopewa na taji la mis temeke na chang'ombe

    ReplyDelete
  12. Aibu hii isiishie kwa Sitti pekee, Lundenga na hao majaji walio husika kumpitisha inatakiwa wawajibike. Ikiwezekana mashindano yasiratibiwe na Lundenga tena, bali iwepo taasisi rasmi inayotambulika na serikali. Reeds wajiangalie mara mbili, kufadhili vitu vivyoo jaa ujanja na upotoshaji kwenye jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...