Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na ujenzi wa mradi mkubwa wa kituo cha  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zimetolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.

Kwa mujibu wa Profesa Shaban Mlacha,amesema kuwa kituo hicho kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi /Utafiti na Tiba, yakiwemo ya figo,akaongeza kusema kuwa kina maabara ya kisasa na vifaa vya kisasa huku kukiwa na vyumba 40 vya madaktari.

Profesa Mlacha amesema kuwa ,kuwapo kwa kituo hicho kitakachojengwa na kukamilika, kitachangia si tu katika kufanya utafiti wa magonjwa na kutibia lakini pia itatoa nafasi kwa wanafunzi wa kitivo cha tiba UDOM na walimu wao kufanya mazoezi yanayostahili na kuonesha ubingwa wao.  

Baadhi ya Wahariri wa Habari kutoka nyombo mbalimbali hapa nchini,wakitoka nje ya Jengo la kituo cha  uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya binadamu katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM),kama kionekanavyo pichani.Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Chuo  hicho  cha  Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha amesema kuwa Ujenzi wa kituo hicho uko katika hatua za mwisho kukamilika na kuwa kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mnamo januari 2015  mwakani .Mradi huo umegharimu kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36 zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa kituo hicho cha kisasa kilichopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa kituo hicho cha kisasa kilichopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. TWILA KAMBANGWANovember 13, 2014

    sawa, pandeni miti sasa si mnaona kiangazi hicho? na pia itasaidia kupatikana kwa mvua ardhi kavu hiyo sio mnapanda viji maua

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...