1
Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi na Matibabu ya magonjwa ya binadamu kinachojengwa katika Chuo Kikuuu cha Dodoma (UDOM)  kikiwa katika hatua za mwisho mwisho za kukamilika.

Kituo hiki kitahudumia wagonjwa kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya jirani ya na mkoa wa Dodoma na kinajengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 ambazo zimetolewa na mfuko huo kwa  silimia 100.

 Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali wanaohudhuria kongamano la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya linalofanyika kwenye hoteli ya Dodoma mjini humo walipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.

Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Mlacha Shaaban amesema “Kituo hiki kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya uchunguzi na utafiti  pia kitatoa wataalamu kutoka katika kitivo cha afya cha Chuo kikuu cha UDOM na wataalamu watakaofanya kazi katika kituo hicho watakuwa wakifundisha wanafunzi na kuhudumia wagonjwa. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma ifikapo Januari 2015"
2
Jengo la kituo cha Utafiti na tiba cha UDOM kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF.
3
Kaimu Makamu Mkuu wa chuo Kikuu cha UDOM Profesa Mlacha Shaaban akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali walipotembelea ujenzi wa kituo cha Tiba na Utafiti kinachojengwa katika chuo kikuu cha UDOM.
4
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Raphael Mwamotoakizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo hicho
5
Waandishi wa habari wakisubiri kupata  maelezo ya kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kituo hiki kitasaidi sana kikitumika vizuri kufanya utafiti wa kisasa wa tiba za wanadamu.

    ReplyDelete
  2. Huko Dodoma wagonjwa kutoka mikoa mbalimbali nchini watakifikia vipi hiki kituo wakati tunajua Dodoma haina uwanja wa ndega? Muache utani serikali kama mnataka kituo hiki kiwe na manufaa kwa wananchi wote uwanja wa Kilakala uanze kujengwa ili Fastjet iende Dodoma pia!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...