Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia leo tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu wa Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika hapo kesho.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt. Kenneth Kaunda mara baada ya Kuwasili katika Viwanja vya Bunge kushiriki Misa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Poleni sana Wazambia wote kwa msiba wa kuondokewa na Rais wenu Michael Sata. Nachukua nafasi hii kuwaomba pia mzidi kuutambua kwa karibu mchango wa Rais wa kwanza wa Taifa lenu la Zambia Dr Kenneth Kaunda. Bila ya mchango wake uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika sidhani kama ungepatikana haraka na uhuru wa Zambia ungekuwa hatarini.

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  2. Nimefunguka. Tanzania inawezekana tukawa tunaelekea kuzuri. Naona wazambia wanachanganya dini na siasa. Padri generali.

    Msiniponde kama mwaona mfumo mzuri toeni maoni kwenye katiba ili na tz iige.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana majirani na Ndg zetu Wazambia kwa msiba huu mzito. Msiba huu uwe kiunganishi zaidi katika umoja wenu wa kitaifa. Enzini mazuri yote ambayo japo kwa muda kidogo Mzee Satta aliyapigania hususani uadilifu na uwajibikaji.

    Nasi Watanzania tuko pamoja nanyi ndiyo maana siyo tu kwa kofia ya SADC bali pia kwa Undugu wetu na ninyi mnamuona Mama Anne Makinda akiwa nanyi katika huzuni.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana jirani zetu kwa msiba huu mzito.
    Kweli mdau hapo juu na mimi nimeona serikali imechanganywa na dini. Ila kama wanaweza kuyamudu yote hakuna shida. Tatizo linakuja pale wanaposhindwa kutofautisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...