Serikali ya China imelaani vikali uzushi uliotolewa na vyombo vya magharibi kutuhumu ndege ya Rais huyo kutumika kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.

Akizungumza leo mjini Arusha Balozi wa China Lu Youqing alisema kuwa huo ni uongo mkubwa ambao ulikuwa na nia ya kutia aibu taifa lake na Tanzania kwa ujumla.

Alisema kwamba Taifa lake hutoa adhabu kali kwa mtu anayefanya uovu kama ujangili, "Kama mwandishi angeweza kuthibitisha hao maafisa wangechukuliwa hatua kali, na hilo liko ndani ya uwezo wangu kwanini ameshindwa kuwataja?"

Lu alisema kwamba Adhabu kama hiyo si kwa mtu aliyekutwa na nyara tu bali hata kwa muongo, "Mwandishi huyo ni muongo na anatakiwa aadhibiwe".

Waziri wa maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu aliunga mkono kauli hiyo na kusema kuwa ilikuwa na nia ya kuchafua hali ya hewa kutokana na mkutano wa kimataifa ulioanza leo jijini Arusha.

"Hata tulipokwenda na rais Kikwete jijini London kwa mkutano wa kimataifa juu ya ujangili gazeti la Dail Mail lilitoa habari za kashfa kuhusu Tanzania siku moja kabla ya mkutano na hii leo ndio limetokea"

Alisema nashukuru wadau wa uhifadhi ambao kwa kiwango kikubwa wamehudhuria kikao chetu muhimu cha leo ambacho kitaleta mabadiliko makubwa katika vita dhidi ya ujangili.

Kikao hichio kilihudhuriwa na mawaziri kutoka nchi tisa za Afrika ukanda wa bahari ya Hindi na afrika mashariki na Kati pamoja na wawakilishi wa mashirika mbalimbali na balozi wa nchi nyingi wanaowakilisha nchi zao.
Balozi wa China nchini Tanzania,Mh. Lu Youqing akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha leo juu ya tuhuma za kuhusishwa kwa Ndege ya Rais wa China kubeba meno ya ndovu kutoka nchini.Katikati ni Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu na kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii,Mh. James Lembeli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nakubaliana na Balozi wa China na sasa tumeona waziri Membe amekubali kuwa mwandishi ni mchafuzi anayeweza kutumia na nchi zinamwonea wivu Mchina jinsi anavyokubalika katika nchi za Afrika katika kuleta mirdi ya maendeleo, na yeye akapata malii ghafi, kufa kufaana..
    lakini kila mara nasoma ahabari za kusema kuwa China inaibia bara la Afrika, sio kitu cha kweli..hawa jamaa wanaleta maendeleo na tumoena bara bara na miumndo mbinu nyingine alizoleta China kwa tanzania na hasa Kenya.
    Bra China China

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...