Na Dotto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog

SERIKALI imesema gharama za kutibu mgonjwa wa kisukari kwa mwaka hapa nchini ni sh.408,000 na kuwa watu wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa huo bila ya wao kujitambua.

Imeelezwa kuwa utafiti uliofanya mwaka 2012 katika wilaya 50 nchini ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya watu huugua ugonjwa huo bila wenyewe kujua.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Afya Kebwe Stephen wakati akitoa tamko la serikali kuhusu siku ya ugonjwa huo ambayo itaadhimishwa duniani kote kesho alisema ugonjwa huo umekuwa na changamoto kubwa kwa vile hutokana na ulaji usiofaa.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye kisukari mwaka huu 2014 ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wote kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki nchini.

"Maadhimisho ya siku ya kisukari yataadhimishwa katika  hospitali zote za Rufaa, mikoa na ngazi  za wilaya kwa wananchi wote  kupima bure sanjari na kupata dawa,"alisema Kebwe.

Alisema watu wengine wanakuwa na dalili lakini huwa hawachukui hatua za mapema ili kuweza kuuzia ugonjwa huo kuendelea.

Alisema dalili za ugonjwa wa kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni kusikia njaa kila wakati,kukojoa mara kwa mara,kupungua uzito, na mwili kukosa nguvu. 


Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2014 ni "Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi" na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa ili kuepuka matatizo mbalimbali yanyotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii. 


 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo mchana , wakati akitoa tamko la serikali kuhusu Siku ya Kisukari Duniani itakayoadhimishwa duniani kesho.
 Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk.Ayoub Magimba (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen kuzungumza na wanahabari.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. Sijenunu Aaron (kushoto) na Mratibu wa Kisukari wizarani hapo, Dk.Auson Rwehumbize wakiwa kwenye mkutano huo.
 "Hii picha ni lazima niipate"  ni kama anaongea Halima Kambi mpiga picha wa Kampuni ya The Guardian Limited wakati Naibu Waziri Kebwe Stephen alipokuwa akitoa tamko hilo kwa wanahabari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...