Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendesha mafunzo ya
kuwajengea uwezo wawezeshaji wa utambuzi wa kaya maskini katika halmashauri
kadhaa nchini. Zoezi hilo ni mwendelezo wa jitihada za TASAF za kunusuru
kaya maskini nchini zoezi lililoanza mwaka uliopita kwa awamu katika maeneo
mbalimbali nchini.
Miongoni mwa halmashauri ambako mafunzo hayo yanafanyika ni
wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa ambako wawezeshaji hao watashiriki katika
kuwapa mafunzo wadodosaji watakaofanya kazi ya tathmini itakayowezesha kutambua
kaya maskini katika vijiji vipatavyo 94.
Zifuatazo ni picha za washiriki wa mafunzo hayo
yanayoendeshwa na TASAF.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini inayoendeshwa na TASAF.
Baadhi
ya washiriki wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika eneo la
utekelezaji la wilaya ya Mufindi wakimskiliza mwezeshaji wa warsha
(hayupo pichani).
Mmoja
wa wawezeshaji katika warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji ngazi ya
halmashauri ya wilaya ya Mufindi akiwasilisha mada.
Mtaalamu
wa ushauri wa TASAF katika halmashauri ya wilaya ya Mufindi ,Lawrence
Mwakitalu akitoa mada kwenye warsha ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa
ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
washiriki
wa warsha ya utambuzi wa kaya maskini katika wilaya ya Mufindi mkoani
Iirnga wakimsikiliza mwezeshaji wa warsha hayupo pichani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...