Jengo la ofisi ya Mkuu a mkoa wa Kilimanjaro linavyoonekana kwa juu.
Katikati ya mji wa Moshi
Jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi linavyoonekana kwa juu.
Eneo la kati jirani na ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.
Ujenzi wa jengo jipya la Ghorofa jirani kabisa na kipta shoto cha Arusha.
Eneo la katikati ya mji wa Moshi.
Jengo zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro .
Eneo la Shanty town linavyoonekana kwa mbali.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii
kanda ya kaskazini.
Moshi looks beautiful and a well organized city. Thank you for the pictures.
ReplyDeleteSasa baada ya kuangalia picha zote nataka kwenda nyumbani kabla ya X-mass! naona kama X-mass ni mbali! Asante kwa picha mangi!
ReplyDeleteAsante sana kwa picha. Umenikumbusha nyumbani na miti ya Xmas imeanza kuchanua.
ReplyDeleteBeautiful city just needs asphalts.
ReplyDeleteMoshi iwe jiji kwa vigezo gani?
ReplyDeleteJiji au small town mbona naona miti zaidi kuliko majengo au macho yangu.show more buildings to justify city status.
ReplyDeleteyote tisa umeacha kulizungumzia JOTO..
ReplyDeleteni kali utadhani tuko Sudan
mdau:- Tango Mike - Arusha
Safi sana mchangiaji wa mwisho na mama nasisitiza Moshi iwe jiji kwa vigezo gani?
ReplyDeleteMoshi haijafikia kiwango cha kupewa hadhi ya jiji. Hata ukiangalia picha zote zimepigwa kwa juu, hakuna hata picha moja inayoonyesha vizuri mji wa Moshi. Kwa ujumla Moshi bado haina hadhi ya kuwa jiji, iendelee kuwa Manispaa tu.
ReplyDeleteMimi nafurahia picha zinaonyesha watu wanatunza mazingira. Miti kibao nyumba chache.
ReplyDeleteAibu aibu aibu,wachangiaji wengi hapo juu kasoro mmoja tu wanazungumzia kuwa Moshi haufai kuwa jiji tu kwa sababu eti miti ni mingi kuliko majengo!!!hivi kweli hadhi za majiji ni majengo?tunasahau kabisa swala la mazingira,mji usio na miti au sio kijani haupendezi hata kidogo hauna afya na hauko hai.Kuna ubaya gani kama Moshi itakuwa jiji na hayo maghorofa mnayoyataka yakajengwa bila kukata hiyo miti?itakuwa ni mfano mzuri kwa kulinda mazingira na kwa unadhifu.Uzuri wa miji siyo majengo pekeyake ni uwiano wa majengo yanayozungukwa na hali ya ukijani ikiwemo miti.Moshi,msikate hata mti mmoja muonyeshe uzuri wa nature,na muwe mfano wa kuigwa.
ReplyDeleteHaya nimewasikieni nyote,
ReplyDeleteWatu wanaacha kuchangia kwa nia nzuri wanaponda tu kwa sababu labda wanatokea miji ambayo haifikiriwi hata kuwa jiji, Mbeya kuna maghorofa gani mpk wakapewa hadhi ya jiji, Tanga kuna maghorofa gani mpka wakapewa hadhi ya jiji na katika vigezo vya jiji hakuna suala la majengo marefu. Ok mpiga picha amepiga picha maeneo ambayo hayana majengo coz naona amepiga kutoka jengo jipya la NSSF Aga khan road ila majengo yanayojengwa ni mengi sana. Wataalamu walisema suala la ukubwa ndio kikwazo cha Moshi kuwa Jiji ila manispaa imeshatatua na ni muda wa Moshi kuwa Jiji mtake msitake.
ReplyDeleteWatu wasichangie kwa bifu coz wanatoka miji isiyofikiria kuwa na hadhi ya jiji ila tuchangie kwa upendo na kweli, Tanga na mbeya hazina majengo mnayoyasema lakini zimepewa hadhi ya jiji kwa mfano mwaka jana mbeya ndio wamepata jengo la kwanza lenye lift wakati Moshi ndio mji wa kwanza wenye jengo lenye lift KNCU najua hiyo ulikuwa hujui. Mpiga picha amepigia sehemu ambayo haina majengo sana ila kuna majengo mengi na project kibao za majengo zinakuja, mfano kuna Jengo na NSSF kubwa sana limejengwa, NHC nao wanatarajia kujenga jengo kubwa sana la kibiashara, emslies wanajenga twin towers za ghorofa 10 10, kuna kibo tower ghorofa 10, kuna majengo ya watu binafsi zaidi ya 12 yanajengwa marefu tu. Hadhi ya jiji haiji kwa majengo kuna vigezo vyake ni vingine. Moshi kigezo kilichokuwa kinaibania ni ukubwa wa eneo ila wameshaipatia ufumbuzi wanaongeza eneo na hatimae soon Moshi will become City.
ReplyDelete