Jengo la ofisi ya Mkuu a mkoa wa Kilimanjaro linavyoonekana kwa juu.


Katikati ya mji wa Moshi


Jengo la ofisi ya mkuu wa wilaya ya Moshi linavyoonekana kwa juu.


Eneo la kati jirani na ofisi za mkuu wa wilaya ya Moshi.


Ujenzi wa jengo jipya la Ghorofa jirani kabisa na kipta shoto cha Arusha.




Eneo la katikati ya mji wa Moshi.


Jengo zilipo ofisi za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro .


Eneo la Shanty town linavyoonekana kwa mbali.Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Moshi looks beautiful and a well organized city. Thank you for the pictures.

    ReplyDelete
  2. Sasa baada ya kuangalia picha zote nataka kwenda nyumbani kabla ya X-mass! naona kama X-mass ni mbali! Asante kwa picha mangi!

    ReplyDelete
  3. Asante sana kwa picha. Umenikumbusha nyumbani na miti ya Xmas imeanza kuchanua.

    ReplyDelete
  4. Beautiful city just needs asphalts.

    ReplyDelete
  5. Moshi iwe jiji kwa vigezo gani?

    ReplyDelete
  6. Jiji au small town mbona naona miti zaidi kuliko majengo au macho yangu.show more buildings to justify city status.

    ReplyDelete
  7. yote tisa umeacha kulizungumzia JOTO..
    ni kali utadhani tuko Sudan

    mdau:- Tango Mike - Arusha

    ReplyDelete
  8. Safi sana mchangiaji wa mwisho na mama nasisitiza Moshi iwe jiji kwa vigezo gani?

    ReplyDelete
  9. Moshi haijafikia kiwango cha kupewa hadhi ya jiji. Hata ukiangalia picha zote zimepigwa kwa juu, hakuna hata picha moja inayoonyesha vizuri mji wa Moshi. Kwa ujumla Moshi bado haina hadhi ya kuwa jiji, iendelee kuwa Manispaa tu.

    ReplyDelete
  10. Mimi nafurahia picha zinaonyesha watu wanatunza mazingira. Miti kibao nyumba chache.

    ReplyDelete
  11. Aibu aibu aibu,wachangiaji wengi hapo juu kasoro mmoja tu wanazungumzia kuwa Moshi haufai kuwa jiji tu kwa sababu eti miti ni mingi kuliko majengo!!!hivi kweli hadhi za majiji ni majengo?tunasahau kabisa swala la mazingira,mji usio na miti au sio kijani haupendezi hata kidogo hauna afya na hauko hai.Kuna ubaya gani kama Moshi itakuwa jiji na hayo maghorofa mnayoyataka yakajengwa bila kukata hiyo miti?itakuwa ni mfano mzuri kwa kulinda mazingira na kwa unadhifu.Uzuri wa miji siyo majengo pekeyake ni uwiano wa majengo yanayozungukwa na hali ya ukijani ikiwemo miti.Moshi,msikate hata mti mmoja muonyeshe uzuri wa nature,na muwe mfano wa kuigwa.

    ReplyDelete
  12. TWILA KAMBANGWANovember 18, 2014

    Haya nimewasikieni nyote,

    ReplyDelete
  13. Watu wanaacha kuchangia kwa nia nzuri wanaponda tu kwa sababu labda wanatokea miji ambayo haifikiriwi hata kuwa jiji, Mbeya kuna maghorofa gani mpk wakapewa hadhi ya jiji, Tanga kuna maghorofa gani mpka wakapewa hadhi ya jiji na katika vigezo vya jiji hakuna suala la majengo marefu. Ok mpiga picha amepiga picha maeneo ambayo hayana majengo coz naona amepiga kutoka jengo jipya la NSSF Aga khan road ila majengo yanayojengwa ni mengi sana. Wataalamu walisema suala la ukubwa ndio kikwazo cha Moshi kuwa Jiji ila manispaa imeshatatua na ni muda wa Moshi kuwa Jiji mtake msitake.

    ReplyDelete
  14. Watu wasichangie kwa bifu coz wanatoka miji isiyofikiria kuwa na hadhi ya jiji ila tuchangie kwa upendo na kweli, Tanga na mbeya hazina majengo mnayoyasema lakini zimepewa hadhi ya jiji kwa mfano mwaka jana mbeya ndio wamepata jengo la kwanza lenye lift wakati Moshi ndio mji wa kwanza wenye jengo lenye lift KNCU najua hiyo ulikuwa hujui. Mpiga picha amepigia sehemu ambayo haina majengo sana ila kuna majengo mengi na project kibao za majengo zinakuja, mfano kuna Jengo na NSSF kubwa sana limejengwa, NHC nao wanatarajia kujenga jengo kubwa sana la kibiashara, emslies wanajenga twin towers za ghorofa 10 10, kuna kibo tower ghorofa 10, kuna majengo ya watu binafsi zaidi ya 12 yanajengwa marefu tu. Hadhi ya jiji haiji kwa majengo kuna vigezo vyake ni vingine. Moshi kigezo kilichokuwa kinaibania ni ukubwa wa eneo ila wameshaipatia ufumbuzi wanaongeza eneo na hatimae soon Moshi will become City.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...