Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa tatu kushoto) sehemu ya msaada wa vifaa tiba vya hospitali vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania vyenye thamani ya shilingi Mil. 20 vitakavyotumiwa katika hospitali hiyo leo Novemba 19,2014,Zanzibar. Makabidhiani hayo yamefanyika kufuatia muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania ya TRA yenye Kauli mbiu isemayo Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" .Wa pili ni Kaimu Kamishna wa TRA (Zanzibar),Mcha Hassan Mcha akiwa pamoja na maofisa wengine wa TRA.Picha na Othman Michuzi.
Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa tiba vya hospitali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib,leo Novemba 19,2014,Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa pili kushoto) akizungumza wakati akitoa shukrani zake kwa Uongozi mzima wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutoa msaada wa vifaa tiba kwenye Hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.
Sehemu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa hospitali ya Mnazi Mmoja,Zanzibar leo Novemba 19,2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...