Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana, Jumatatu, Novemba 10, 2014, alianza kuwasiliana na mamia kwa mamia ya wananchi mbali mbali nchini kujibu ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wa kumpa pole, kumtakia heri na nafuu ya haraka ambao amekuwa anatumiwa na wananchi tokea mwishoni mwa wiki.

Tangu alipofanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostrate) Jumamosi iliyopita kwenye Hospitali ya Johns Hopkins, Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, Rais Kikwete amepokea mamia kwa mamia ya SMS zikimpa pole na kumtakia nafuu ya haraka.

Rais Kikwete bado anaendelea kujibu SMS hizo na wananchi ambao wamemtumia SMS Rais Kikwete waendelee kusubiri majibu ya Mhe. Rais kwa sababu anakusudia kujibu SMS zote ambazo ametumiwa.

Aidha, Rais Kikwete jana alizungumza kwa simu na uongozi wa juu wa Tanzania kwa mara ya kwanza tokea afanyiwe upasuaji. Rais alizungumza na Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda.

Wakati huo huo, madaktari wanaondelea kumtibu Rais Kikwete jana waliondoa bandeji kwenye sehemu ambako alifanyiwa upasuaji wakieleza kuwa hali yake inaendelea vizuri na anapata nafuu kwa kasi nzuri.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasiliana na baadhi ya wananchi waliokuwa wakimjulia hali kupitia simu yake ya mkononi kupitia ujumbe mfupi(sms) leo Jumatatu.Rais Kikwete anayepata matibabu katika hospitali ya Johns Hopkins jijini Baltimore Maryland nchini Marekani anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mara kwa mara na afya yake inaendelea kuimarika(picha na Freddy Maro)

Mwisho.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
11 Novemba,2014


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Inabidi apumzike. Ni vizuri kuwasiliana na watu Ila he needs rest and a stress free environment in order to recuperate. Wishing him a speedy recovery.

    ReplyDelete
  2. Ukitaka number yake unaipataje maana na sisi wengine tunataka kumpa pole na nakumtakia afya njema

    ReplyDelete
  3. Safi kabisa mdau wa kwanza. Inabidi apumzike kwanza

    ReplyDelete
  4. upone haraka kwa jina la Yesu. Ila kwenye taarifa naona kuna typo, ni prostate sio prostrate kama alivyoandikwa.

    ReplyDelete
  5. Mwenye number ya Mh. Rais tunaomba basi ili tumpe pole na sisi jamani.

    ReplyDelete
  6. I wish him quick recover

    ReplyDelete
  7. hata sisi wa mbagala tunahaki ya kumjulia rais hali/pole,FREDDY MARO tunaomba namba ya rais,
    maana wakati wa kupiga kura tunashiriki wote,basi hata kuwa na namba wote tuijue.

    ReplyDelete
  8. POLE SANA MHESHIMIWA RAIS,TUNAKUOMBEA MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU UPONE HARAKA.WADAU MWENYE NAMBA YAKE ANIPATIE ILI NIMTUMIE SMS.

    ReplyDelete
  9. Namba ni hii kwa yoyote anayeta kumusms mheshimiwa rais kwa simu yake ya kiganjani ni +16463092295

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...