Mwenyekiti wa Chama cha UPDP na aliyekuwa mbunge wa bunge maalum la katiba Mh. Fahmi Dovutwa akitoa taarifa ya ushirikiano wa Vyama sita vya siasa visivyokuwa na wambunge katika uchaguzi wa Serkali za Mitaa, Wabunge na Rais unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu mpaka mwaka 2015 ambapo uchaguzi wa Wabunge na Rais utafanyika.

 Mhe Dovutwa amesema vyama hivyo vimeamua kushirikiana kwa sababu vipo vyama vilivyounda kundi lisilokuwa la kisheria linaitwa Ukawa, lakini  hakuna sheria inayoturuhusu kuunganisha vyama ila tunaweza kushirikiana tu ndiyo maana tunasema tumekubaliana kushirikiana”. vyama vilivyokubaliana kushirikiana ni SAUT, DEMOKRASIA MAKINI, JAHAZI ASILIA, UMD, UMD, UPDP NA AFP ,  Katika picha wanaofuatia ni Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Rashid Lai Katibu Mkuu AFP na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa.
 Rashid Lai Katibu Mkuu AFP akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika Sinza jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Yusuf Manyanga , Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa na Dominic Lyamchai Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini
Mwenyekiti wa Chama cha SAUT  Mhe Yusuf Manyanga  akifungua mkutano huo kabla ya Mwenyekiti wa UPDP Mh. Fahmi Dovutwa kutoa tamko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vyama kama hivi vinavyojitokeza wakati wa uchaguzi tu vinafaa vifutwe maana inaoneka vinatafuta pesa za ruzuku tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...