Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Siha ,Rashid Kitambulilo akimuongoza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama wakati akitembelea eneo la mwekezaji la Tanganyika Film and Safari ambako wafugaji jamii ya Masai wanadaiwa kufanya uharibifu mkubwa.


Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wakitizama uharibifu  uliofanywa na wafugaji jamii ya Masai.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akitizama moja ya gari lililochomwa moto na watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji jamii ya Masai.
Uharibifu mkubwa umefanyika ambapo nyumba 16 na magari tisa yameteketea moto.
Mwekezaji Peter Jones akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo lililomsababishia hasara kubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Maswala ya wawekezaji na wenyeji yapatiwe ufumbuzi wakati yanapojitokeza. Yasingoje mpka chuki kiasi hiki imeshajengeka na uharibifu wa mali na hasara kiasi hiki itokee hii haisaidii.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la watendaji wetu wanasubiri mpaka yatokee madhara ya watu kupoteza maisha na kama hayo yaliyotokea ndipo wanaanza kushughulika. BADILIKENI, chukueni hatua kabla ya hatari

    ReplyDelete
  3. Sawa sawa tu, maana viongozi wetu madudu matupu.walichokifanya nakiunga mkono

    ReplyDelete
  4. sawa sawa na kama inawezekana wafanye tena, hakuna wawekezaji wala nn wezi wote. kaunzia ngazi za juu mpaka wanaokuja kuiba mbwa tu

    ReplyDelete
  5. walipokufa watu kwenye mapigano wala hakuna aliyejigusa .... mpaka jana tunamuona IGP huko na PM akitoa taarifa huku yuko DODOma .... mwekezaji kavamiwa tu viongozi wa serikali ya mkoa wala hawajachelewa kufika eneo la tukio

    haya matatizo yanatoke a kwa sababu serikali inazidi kuwaondoa hao wafugaji wa kimasai kwenye maeneo yao huko mbugani wanakosa malisho na kuanza kuvamia maeneo ya wakulima na raia wengine .... tatizo la wafugaji litafutiwe ufumbuzi!!!

    ReplyDelete
  6. Hakuna hasara hapo. Wamemwongezea hela tu mwekezaji, hizo mali zote zina bima atalipwa mara 100. Kuna mwekezaji mmoja zanzibar ana duka la kuuza pombe. Kila mwaka linachomwa. Sasa watu wanauziza huyu hafungi tu duka lake? Hakuna kitu cha hicho jamaa baada ya wiki nne tu duka huwa linafungiliwa tena na vitu zaidi ya mwanzo, bima inalipa na mkutajirisha tu jamaa. Same thing here huyu jamaa atalipwa mabilioni anakuja tena "kuwekeza"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...