Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kuranga wakati walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo wilayani hapo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila na mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza na Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. Kushoto ni mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete.
Mkutano ukiendelea kabla ya wageni kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Msufini Kidete iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...