Itakumbukwa katika mkutano
uliofanyika mapema mwezi huu jijini "CAIRO" hofu
ya ukuwaji wa uhalifu mtandao unaoweza kurudisha nyuma uchumi wa mataifa ya
Afrika ulipata kujadiliwa kwa kina huku nchi ya Misri ikionyesha
washiriki wa mkutano huo jitihada inayoendelea nayo katika kukabiliana na
uhalifu mtandao.
Ime ripotiwa na Mtandao wa "MGAFRICA" kuhusiana
na kilichojiri katika mkutano uliokamilika jijini Johannesburg, Afrika kusini
wa maswala ya usalama mitandao ambapo Bara la Afrika limetabiriwa kuwa na
ukuaji wa uhalifu mtandao kutokana na mikakati daifu ya kujiweka salama huku
ikiwapatia wahalifu mtandao urahisi mkubwa wa kuleta maafa siku za usoni.
Kumeendelea kuwa na wimbi
kubwa la uhalifu mitandao ingawa jitihada za kukabiliana na uhalifu huo
zimeendelea kugharimu mataifa mengi hivi sasa. Mataifa yamekua yakiwekeza
kwenye maswala ya usalama mitandao lakini bado wahalifu mtandao wameonekana
kuendelea kutamba.
|
Home
Unlabelled
WAHALIFU MTANDAO WATEGEMEWA KUELEKEZA NGUVU ZAO BARANI AFRIKA - WATAALAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...