Mtu mmoja ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje na mkono wake kukatika alipotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa doria usiku wa kuamkia leo na kujeruhi askari polisi wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa watu wa nne waliokuwa na mtu huyo wamekimbia huku polisi wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo na kwamba hili ni tukio la tatu la mabomu dhidi ya askari Polisi na amasema kukamatwa kwa simu hizo ni mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini Songea.
Mkuu huyo amesema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini CP Isaya Mungulu anafanya safari kuja Songea leo na atazungumza na vyombo vya habari.
Mwandishi wa habari hii aliyekuwepo eneo la tukio aliweza kushuhudia mabaki ya bomu hilo pamoja na mzula wa kuziba sura aliokuwa akiutumia mtu huyo.

CHANZO: ITV

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...