BAN KI MOON
ATAKA USHIRIKIANO ZAIDI BAINA YA UMOJA
WA MATAIFA NA UMOJA WA AFRIKA
·
NI KATIKA ENEO LA OPERESHENI ZA
ULINZI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon, akizungumza wakati wa majadiliano
kuhusu ajenda ya ushirikiano
baina ya Umoja wa Mataifa na
Umoja wa Afrika katika eneo la
Operesheni za Ulinzi. Majadiliano hayo
yamefanyika siku ya Jumanne.
Na
Mwandishi Maalum, New York.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki Moon, amesema,
ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa
na Umoja wa Afrika katika operesheni za
ulinzi wa Amani umekuwa wa mafanikio makubwa katika urejeshwaji wa hali
ya amani na utulivu katika maeneo yenye
migogoro. Hata hivyo amesema pamoja na mafanikio hayo kuna umuhimu wa ushirikiano huo kuboreshwa zaidi
na kuwa wenye tija .
Alikuwa akizungumza wakati wa majadiliano ya wazi ya siku moja juu ya ajenda ya Operesheni za Ulinzi wa Amani, mkazo mkubwa ukielekezwa zaidi katika
ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na
Umoja wa Afrika. Majadiliano hayo ambayo pamoja
na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, pia mshiriki mwingine alikuwa Rais Mstaafu wa Burundi, Pierre Buyoya ambaye
ni Mjumbe Maalum wa AU huko Mali na Ukanda wa Sahel. Yameandaliwa na Baraza
Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo kwa mwezi huu wa Desemba lipo
chini ya Urais wa Jamhuri ya Chad.
Ban Ki Moon ameeleza kuwa kwa miaka mingi ushirikiano kati ya UM na washirika wake wa Kikanda umezidi kuimarika na kwamba Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa na
Baraza la Amani na Usalama la
Umoja wa Afrika yamekuwa yakifanya kazi kwa karibu zaidi.
Amesisitiza kuwa ni kutokana na
ushirikiano huo, kumekuwapo na
uongezeko la uungwaji mkono wa operesheni za kulinda Amani ambazo zimekuwa
zikifanyika chini ya Umoja wa Afrika.
Akizungumzia zaidi kuhusu ushirikiano
huo na mafanikio yake, Ban Ki Moon amebainisha
kwamba, katika Kanda ya Maziwa Makuu, ushirikiano baina ya
Umoja wa Mataifa, Umoja wa
Afrika, Mkutano wa Kimataifa wa Nchi za Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo
ya Nchi za Kusini mwa Afrika umesaidia
sana katika kurejesha hali
ya utulivu katika DRC na eneo la
Maziwa Makuu.
Akaeleza pia kuwa huko Somali taasisi hizo mbili kwa maana ya
UM na AU pamoja na wadau wengine wanafanya kazi kwa karibu katika
kuisaidia serikali ya shirikino ya nchi hiyo katika hatua muhimu ya ujenzi wa Amani na ujenzi wa taifa
la Somalia. “ pia tunafanya kazi kwa karibu na AU na Taasisi zingine za Kikanda
huko Sudan na Sudani ya Kusini katika
suala zima la kutafuta Amani na usalama wa kudumu katika maeneo hayo”.
Amesema Katibu Mkuu.
Na kusisitiza kuwa pamoja na kuwapo kwa mafanikio bado
kuna umuhimu kwa kuongeza juhudi
zaidi katika eneo hilo la ushirikiano na hasa kutokana na ukweli kuwa walinzi wa
Amani wanaohudumu katika Taasisi hizo wanakabiliwa na changamoto nyingi na
hatari kubwa zaidi.
Ban Ki Moon, ameleza kuwa walinzi hao wa Amani wanafanya kazi katika mazingira
magumu na hatarishi huku wakilazimika
kukabiliana na makundi ya waasi wenye silaha, makundi ya kigaidi na makundi ya uhalifu wa kupangwa.
Na kwa sababu hiyo anasema ili kuboresha ushirikiano uliopo baina ya UM na AU panahitajika mbinu na fikra mpya na mbadala zitakazokwenda sambamba na mabaliliko
yanyojitokeza hivi sasa katika eneo hilo la operesheni za ulinzi wa
Amani.
Aidha anasema panahitajika si tu ushirikiano wa kisiasa bali pia uwepo wa
uwazi, uwajibikaji na vile vile kujua nani anafanya nini wapi na kwa wakati
gani na majukumu ya kila Taasisi. Akasisitiza kuwa Jumuiya ya Kimataifa inatambua vema kuwa
migogoro inayoikuba si matatizo ya
Afrika peke yake bali inahusu
Jumuiya yote ya Kimataifa na kwamba utatuzi wake
unahitaji ushirikiano wa pamona na kufanya kama kama kitu kimoja.
Akizungumzia kuhusu Afrika kuwa na vyanzo vyake vya mapato vitakavyogharamia
shughuli za ulinzi, Ban Ki Moon amesema inagaya naye amekuwa muumini wa dhana hiyo lakini bado anaamini kuwa mchango
wa Jumuiya ya Kimataifa unahitajika pia. Akaushukuru Umoja wa Afrika kwa namna ambavyo imekuwa ikishughulikia
migogoro mbalimbali inayojitokeza katika Afrika pamoja na ushirikiano wake na
Umoja wa Mataifa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...