Anchali Seleman Mmoja wa wakulima wa mpunga katika bonde la Madibira
akiandaa mbegu ya mpunga katika kitalu chake baada ya kuwezeshwa na
udhamini wa Baraza la Uwezeshaji Taifa kupitia bank ya CRDB pamoja na
Madibira Saccos.
Baadhi ya wakulima waliodhaminiwa na serikali kupitia
baraza la uwezeshaji la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na
wawakilishi kutoka baraza hilo.
Mmoja ya Mkulima aliyefanikiwa kupata udhamini wa baraza la uwezeshaji
akielezea mafanikio yake baada ya udhamini huo ikiwa pamoja na ujenzi wa
nyumba ya kisasa na kununua trekta na vifaa kazi vingine.(Picha na
Denis Mlowe).
NA DENIS MLOWE, MADIBIRA
BARAZA
la uwezeshaji Taifa limewanufaisha jumla ya wakulima 400 wa kilimo cha
Mpunga wa bonde la Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa
kuwadhamini kupitia benki ya CRDB tawi la Iringa na Madibira Saccos
baada ya kupatiwa mkopo wa shilingi milioni 400 ambazo zimeweza
kuwanufaisha katika kilimo cha mpunga kwa kununua vifaa vya kilimo na
kukuza kipato.
Akizungumza
na Tanzania Daima wakati walipowatembelea wakulima hao na kufanya
ukaguzi wa udhamini huo mwishoni mwa wiki, Afisa Mwandamizi Mawasiliano
ya Umma na Ushawishi kutoka Baraza la Uwezeshaji Taifa, Edward Kessy
alisema kuwa lengo la udhamini wa serikali kwa wakulima hao ni
kutekeleza mpango wa taifa wa matokeo makubwa sasa kuwawezesha wakulima
kuinua kipato chao na kukuza uchumi wa nchi kupitia kilimo.
Kessy
alisema kuwa kupita benki ya CRDB tawi la Iringa serikali wamewadhamini
wakulima hao fedha hizo ambazo wanazikopa kupitia Madibila Saccos
inayofadhiliwa na benki hiyo na wamepatiwa elimu ya kilimo cha kisasa
ambacho kimewasaidia kuongeza uzalishaji mazao na kudhibiti tatizo la
njaa wilayani humo.
“Baraza
la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi chini ya mfuko wake wa
uwezeshaji mwananchi ambao unatekelezwa kwa kushirikiana na benki ya
CRDB imeweza kuwadhamini wajasiriamali mbalimbali kwa
kupitia vyama vya kuweka na kukopa nchini kuweza kupata mikopo ambayo
inakuwa mitaji katika kuendeleza biashara zao na kilimo kwa ujumla na
itaendelea kutoa udhamini zaidi kwa mwaka wa fedha ujao’ alisema Kessy.
Alisema baraza hilo hadi
sasa limeweza kutoa mikopo yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 7
kwa wajasiriamali mbalimbali na wakulima wa mazao mbalimbali na wakulima
wa mpunga Madibira wamedhaminiwa shilingi milioni 400 ikiwa ni awamu ya
kwanza kwa wakulima hao.
Awali
wakulima hao waliishukuru serikali kwa udhamini huo uliowawezesha
kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato cha familia sambamba na kuongeza
mavuno ya mpunga kwa mwaka jana.
Mmoja
wa wakulima wa mpunga katika bonge la Madibila, Anchila Seleman alisema
kuwa mkopo huo umewawezesha kukuza kipato na mavuno ingawa wanakumbana
changamoto ya soko la zao la mpunga hapa nchini.
Alitoa
wito kwa baraza la uwezeshaji kuendelea kutoa mikopo kwa wakulima kwa
lengo la kuwanufaisha na kuwatafutia masoko nje ya nchi kuweza kuuza
mpunga kwa faida tofauti na sasa ambapo soko limekuwa likiwadidimiza
wakulima wadogo.
Kwa
upande wake,Bruno Theodory Meneja Mahusiano wa benki ya CRDB tawi la
Iringa alisema kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa
wakulima hao kupitia mahusiano mazuri waliyoweka na Madibira Saccos
ambapo wakulima hujipatia mikopo kila mwaka kutokana na uanachama
waliokuwa nao.
Alisema
kuwa msimu wa 2013/2014 wakulima walionufaika na udhamini wa baraza la
uwezeshaji ni zaidi ya 400 waliojipatia mkopo wa shilingi milioni 1 kwa
kila mkulima na kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao mengi zaidi tofauti
na misimu iliyopia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...