Mgeni rasmi Waziri wa Kazi na Ajira,
Gaudentia Kabaka, na viongozi wa juu wa PSPF,na TPB, wakiwa katika picha ya
pamoja.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, (TPB), Sabasaba Moshingi, (Wakwanza kushoto) na Balozi wa PSPF, Mrisho Mpoto, wakishikana mikono kuashiria uzinduzi wa huduma mpya za mikopo kwa wanachama wa Mfuko huo kupitia TPB jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi Desemba 11, 2014
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka,
ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, TPB, Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake.
Leo Desemba 11, 2014 Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa
kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania wamezindua huduma mpya kwa
wateja wake, huduma hizo ni Mkopo wa kuazia Maisha na Mkopo wa elimu.
Kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa
ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yoyote ile ya elimu, mfano
stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.
Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 4.
Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, mwanachama aliyepata
ajira kwa mara ya kwanza huwa ana mahitaji muhimu, kwa kutambua hilo
PSPF imeanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaweza kukopa mishahara
yake ya miezi miwili ili aweze kujipanga na maisha mapya ya
ajira. Katika huduma hii PSPF imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.
Lengo kubwa la PSPF kuanzisha mikopo hii ni kuhakikisha
kila mtanzania anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika masomo kwa kupitia
mkopo wa elimu au ndoto yake nyingine kwa kupitia mkopo wa kuanzia
maisha, hivyo natoa wito kwa watanzania wenzetu kujiunga na PSPF ili
waweze kufaidika na fursa hizi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Kazi na Ajira
Mheshimiwa Gaudentia kabaka alisema amefurahishwa na PSPF jinsi
ilivyoshirikiana na Benki ya Posta Tanzania katika Kubuni, Kupanga,
kuandaa na hatimaye kuteleza utratibu huu, alisema hili ni jambo sahihi
na mwafaka kwani kwa mujibu wa taratibu za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
duniani kote, kazi za Mifuko hii sio kutoa mikopo bali ni kuwawezesha
wanachama wake kupata mafao yao stahili pale wanastaafu.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania,
Bw. Sabasaba Moshingi alisema mwanachama wa PSPF anayetaka kukopa
anatakiwa kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya Posta lililopo karibu
yake. Huduma za utoaji wa mikopo hii ni za haraka sana na bora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...