National Arts Council BASATA

Yah: Salaam za
Rambirambi
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa
msanii nguli wa tasnia ya muziki wa Dansi nchini Shem Ibrahim Kalenga
“
Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha
Shem Ibrahim Kalenga ambaye mchango wake katika muziki wa Dansi ni mkubwa mno
na unahitajika sana, pengo aliloliacha
ni kubwa kwani ubunifu wake bado unahitajika katika tasnia hii.” Baraza linatoa
pole kwa familia ya marehemu na wasanii wote nchini, aidha tunawatakia moyo wa
subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Baraza liko pamoja na
familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Imetolewa
na
Godfrey
Mngereza
Kaimu
Katibu Mtendaji
Baraza
la Sanaa la taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...