Na Andrew Chale
WABUNIFU wa Mavazi wachanga na chipukizi wamemwandalia Sherehe za kuzaliwa ya Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin, zitakazofanyika usiku wa Desemba 24, ndani ya ukumbi wa M.O.G Bar (Nyumbani Lounge) huku ikisindikizwa na Spice Modern Taarab pamoja na Mini fashion show.
Katika usiku huo maalum, kiingilio ni sh 5,000, huku vazi maalum likiwa Black & White, ambapo pia wadau watakaojumuika na Mama wa Mitindo, watapata burudani kali ya muziki kutoka kundi hilo la Spice Modern taarab, Dj Mapuu pamoja na shoo ya ubunifu wa mavazi (Min fashion show) itakayopambwa na wabunifu wanaochipukia.
Usiku huo wa Black &White Bash 55th Asia Idarous Khamsin, pia itakuwa na Red Carpet na wadau watapiga picha na mastaa mbalimbali sambamba na pongezi za kunyakua tuzo ya ‘Life Time Achievement Swahili Fashion Week 2014’.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...