Mshiriki  wa Tanzania anayewakilisha ndani ya mjengo wa Big Brother ‘hotshots’ , Idris Sultan ndiye ameibuka kidedea leo usiku katika shindano hilo huko Afrika Kusini. Idris amekuwa Mtanzania wa pili kushinda shindano hilo, baada ya Richard Dyle Bezuidenhout kuibuka kidedea mwaka 2011 katika Big Brother Afrika II.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera sana Idrisa kwa kutuwakilisha WaTz
    wadau
    FFU -Ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Idris kwa ushindi wako mnono BBA. Kwa mara nyingine tena Tanzania imeonekana tena katika ramani ya dunia. Ni hivi juzi tu Diamond Platnumz kajizolea tuzo katika sanaa ya muziki.

    Hongereni sana Idris Sultan na Nasib Abdul kwa kutupeperushia vyema kabisa bendera ya Taifa letu la Tanzania. Mungu awabariki. Nina hakika hata Mhe. JK atakuwa amezidi kupata nafuu kubwa katika maradhi kutokana na furaha aliyonayo kutokana na ushindi wenu, furaha hii ni kubwa sana.

    Mungu Ibariki Tanzania!

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  3. SIO DOLA ELFU TATU (3,000.00) NI DOLA LAKI TATU (300,000.00)

    ReplyDelete
  4. Ingawa mkwanja atachukua Idris na kufaidi yeye na ukoo wake na marafiki :) hakika ushindi huu ni wa kujivunia sisi wote waTanzania, kwani kwa mara nyingine tena tumesikika katika vyombo vya habari vya kimataifa. Umecheza mchezo vyema na HONGERA sana Ndugu Idris

    Kutoka Ughaibuni

    ReplyDelete
  5. TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA TANZANIA

    ReplyDelete
  6. haya tunawasubiri huku na kaka yetu Mwigulu tukate kodi zetu kwenye hicho kipato halali.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana bro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...