Mshambuliaji Danny Mrwanda amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja usiku huu.

Yanga imewafanyia umafia watani zao wa jadi Simba,ambayo ilionyesha nia kubwa ya kumuhitaji Mrwanda ikiwa ni kwa hudi na uvumba na tayari
ilishatangaza nia yake hiyo ya kutaka kumsajili.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi,na mshambuliaji pekee wa ndani wanayemtegemea ni Hussein Javu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Yaani Simba na Yanga hakuna jipya.Danny mrwanda ni mchezaji ambaye ameisha na hana kiwango. Lakini kwa umbumbumbu na ushabiki usio na tija wa viongozi wa Yanga wanaona kama wamemsajili Eden Hazard. Hebu badilikeni.Tafuteni wachezaji vijana hii mitumba ya kusaka mafanikio ya muda mfupi haiwasaidii kitu,Hebu tujiulize Yanga wamemleta Maximo ili awasisdie kujenga kikosi imara chenye mustakbali mzuri?Hawana jipya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...