SAM_0616
Wachezaji wa Tanzania na Kenya wakiwa katika mashindano ya wabunge wa jumuiya ya Afrika mashariki leo,  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Karume jijini Arusha, mechi hiyo ilivuta hisia za wakazi wa jiji hilo waliomiminika kuja kushuhudia wabunge hao wakimenyana uwanjani, baada ya dakika ya tano bunge la kenya walijipatia bao la kwanza, bao lililofungwa na Mh.Steven Nyatta na hatimaye Tanzania kusawazisha dakika ya 24 kwa njia ya penalt baada ya Mh.Mbunge Joshua Nassari kudondoshwa eneo la hatari kwa kugongwa na mlinda mlango wa kenya Kega Kanin.
SAM_0003
Mlinda mlango wa Timu ya kenya Kega Kanin akijaribu kuzuia goli lililopatikana kwa njia ya penalt katika dakika ya 24 .
SAM_0018
Naibu Waziri   wa  Fedha   Adam  Malima akichechemea uwanjani baada ya kuanguka na kupewa huduma ya kwanza.
SAM_0012
Wachezaji wa timu ya Tanzania wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza
SAM_0013
Wachezaji wa timu ya Kenya wakijadiliana uwanjani kabla ya mechi kuanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...