Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Juma Assad na ambaye kwa wadhifa wake ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa akiwa na baadhi wa wasaidizi wake katika Kikao cha Bodi ya Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kilichofanyika jana ( Jumanne) Hapa Umoja wa Mataifa.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwenye tai nyekundu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu kutoka Uingereza aliyekuwa akimkaribisha kwenye Bodi hiyo, upande wa kulia ni Ujumbe wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka India. Uingereza, India na Tanzania ndiyo inayounda Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa na Mashirika yake. Katika mkutano huo ilielezwa kuwa Tanzania kwa maana ya CAG itachukua uenyekiti wa Bodi ifikapo Januari Mosi mwakani, uenyekiti huo ni wa miaka miwili.
Pamoja na Kushiriki Vikao vya Bodi, CAG alipata nafasi ya kufika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ambako alipokelewa na Mwenyeji wake, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Ramadhani Mwinyi. Akiwa katika Uwakilishi wa Kudumu CAG alijionea maendeleo ya ukarabati wa Jengo la Uwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ukirudi kagua kituo cha mabasi ubungo. Tunaibiwa sana.

    ReplyDelete
  2. Du kila sehemu viongozi na washindi sisi tu, sadec sisi, east africa sisi, mahakama ya aicc sisi, au sisi, big brother sisi, channel o sisi, hapo sijataja na mambo mengine na yaliyopita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...