Mmoja wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla.

Globu ya Jamii inaitakia kheri na fanaka Clouds FM katika kusherehekea miaka 15 tangu kuzaliwa kwake.
 Ndafu wa shughuli akiwa mezani
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
 Msanii mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
 Mkuu wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty.
 Dj Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo ya kutimizwa miaka 15 ya kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na kwingineko.
 Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka 15 tangu kuanzishwa kwake nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CloudsFM na CloudsTv, mbona hampatikani tena mtandaoni? Je, mmehamia mitaa gani ya MTANDAO?

    Hata hivyo HONGERENI sana kwa kutimiza miaka 15 ya kuyakata mawingu. Kwa kweli mnastahili pongezi za hali ya juu. Mmeibadirisha Tanzania kutoka chini na kuipandisha juu, inaonekana na dunia nzima na pia mnawajali sana Watanzania katika mambo mengi. Big up people!

    Peters Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...