
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk Titus Kamani akifungua semina ya siku mbili ya kimataifa inayozungumzia makabila ya asili, haki zao na namna ya kuboresha maisha na mifumo ya chakula . Semina hiyo inayofanyika Hoteli ya Kunduchi jijini Dar es Salaam inajiandaa kwa kongamano la dunia nzima kuhusiana na jamii za asili ambalo litafanyika Roma Italia, Februari 2015.
Mwakilishi Shirika la Kimataifa la maendeleo ya Kilimo, IFAD, Bw.Francisco Pichon akisisitiza jambo wakati wa kongamano hilo.
Neno "makabila ya asili" ni sahihi kweli? Kuna makabila ambayo sio ya asili?
ReplyDelete