BENDI nne nyota nchini, FM Academia, Yamoto, Mapacha
na SkyLight zitatumbuiza katika jukwaa moja kwenye
tamasha la Beach band Bonanza lililopangwa kufanyika
Desemba 20 kwenye ufukwe wa Azura, Kawe darajani.
Bonanza hilo limeandaliwa na kampuni ya Team Mamba na
mbali ya bendi hizo nyota, wasanii wa bongo fleva
wakiongozwa na Dully Sykes, CPWAA na Damian Soul
ambaye atakuja na bendi yake.
Msemaji wa kampuni ya Team Mamba, Doris Godfrey
alisema kuwa bonanza hilo lililodhaminiwa Coca-Cola na bia
ya Windhoek, limepangwa kuanza saa 6 mchana mpaka
alfajiri.
Doris alisema kuwa wameandaa bonanza hilo kwa ajili ya
kuwakutanisha wadau wa muziki na familia zao kwani siku
hiyo kutakuwa na michezo ya watoto mchana na baadaye
usiku kwa ajili ya wakubwa.
Alisema kuwa pia kutakuwa na michezo ya watoto, kupanda
farasi na michezo mingine ambayo ni ya kuvutia.
“Hili ni bonanza la kwanza la muziki linalokutanisha bendi
nyingi ambazo zitafanya shoo katika jukwaa moja, hivyo
tunatarajia kuwa na burudani aina yake kwani bongo fleva
nao watakuwepo kwa lengo kutoa burudani safi,” alisema
Doris.
Kiongozi wa bendi ya FM Academia, Nyoshi El Sadaat
alisema kuwa wamejiandaa vizuri kutoa burudani katika
bonanza hilo la aina yake. “Tuna nyimbo mbalimbali mpya,
staili mpya ambazo siku hiyo zitakuwa zinaonyeshwa mara
kwanza jukwaani,” alisema Nyoshi.
Kwa upande wake, Dully Sykes alisema kuwa wamejiandaa
vilivyo kwa ajili ya tamasha hilo na kuwaomba mashabiki wa
muziki kufika kwa wingi.
Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu Beach Band Bonanza litakalofanyika Desemba 20 katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Ilunga Khalifa (Cpwaa) na Mratibu wa Bonanza hilo, Dorice Godfrey.
Mratibu wa Bonanza la Beach Band, Dorice Godfrey akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo kuhusu Bonanza hilo litakalofanyika Desemba 20 katika ufukwe wa Azura jijini Dar es Salaam.Kulia ni Msanii Dully Sykes na kushoto ni Rais wa Bendi ya FM Academia, Nyoshi El Saadat
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...