KIKOSI cha timu ya Friends Rangers (pichani), kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Makurumla, Magomeni Mwembechai, Dar es salaam kuvaana na timu ya Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo wa kirafiki wa kijiandaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza. 
 Ofisa habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kikosi hicho kinashuka dimbani kikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo inayoanza kutimua vumbi Ijumaa ya Desemba 26, 2014. 
 Alisema kwa kutambua umuhimu wa michuano hiyo ambapo wao wataanzia ugenini dhidi ya Lipuli ya Iringa, imejipanga kupata mechi kadhaa za kirafiki, ambapo kesho Jumapili itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Ruvu Shooting. 
Kigundula alisema kuwa kikosi chao kipo katika maandalizi makali ya kuhakikisha kinaendeleza rekodi yake ya kutofungwa kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo. Alisema timu yao chini ya kocha wake Ally Yusuph 'Tigana' kimewasajili Haruna Moshi 'Boban' Amir Maftah, na Robert. Wengine ambao wamekuja kwa mkopo Wine Abbas kutoka Ruvu Shooting na Mahmoud Osman kutoka Coastal Union. 
 "Tunaendelea kukinoa kikosi chetu kwa kupata mechi nyingi za kirafiki lengo letu ni kuendelea na safari yetu ya kupanda daraja, ambapo msimu ujao tunataka kucheza ligi kuu"alisema Kigundula. Friends Rangers inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi daraja la kwanza, huku Majimaji ikishika usukani wa ligi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...