Baada ya kukosekana mvua kwa muda mrefu katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji wa mitim, hali ya zamani imeanza kurejea. |
Majani kwa ajili ya mifugo kwa sasa yanapatikana na hata afya sasa imeanza kurejea tofauti na ilivyokuwa hapo awali. |
Mmoja wa wafugaji Ludovick Meela Serik akifurahia hali ya upatikanaji wa majani kwa ajili ya mifugo yake ilivyo sasa. |
Na Dixon Busagaga wa Globu
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Dah kaka Michuzi uchokozi mwingine!! umenikumbusha kwetu...X-mass ifike haraka niende dahh nimepamiss sana
ReplyDeleteTuendelee kuhifadhi mazingira tusikate miti ovyo, tukilazimika kukata ili tupikie au kujengea tukate mmoja tupande miti kumi, la sivyo tukiharibu vyanzo vya maji hali ya hewa itabadilika na tunaweza kuwa na sehemu zinazogeuka kuwa jangwa ambalo kilimo chake hakitawezekana.
ReplyDeleteHaya sasa ndo maendeleo ya kweli wenyewe wanasema sustainable developments kila pembe ya Tanazania hasa kule kwenye mvua nyingi tujitahidi sana kupanda miti magereza,vyuo,shule,tassis binafsi na watu binafsi panda miti kwa wingi maji yanakauka kwa speed ya kutisha sana,bila shaka kutakuwa na vita ya kugombea maji hasa vijijin muda si mrefu...Tuawaachie watoto wetu nchi ya kijani hongera sana Kilimanjaro
ReplyDelete