Baada ya kukosekana mvua kwa muda mrefu katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji wa mitim, hali ya zamani imeanza kurejea.
Kurejea kwa hali hiyo kumetokana na jitihada za mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ,kushiriki katika utunzaji wa mazingira kwa kuzuia wananchi walioishi jirani na maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro kuingia katika eneo la nusu maili kufanya uharibifu katika misitu ya asili,Mito iliyokuwa imekauka sasa imeanza kutirisha maji kama ilivyokuwa zamani.
Kina mama ambao awali walilazimika kuingia ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya ukatajai wa majani kwa ajili ya mifugo yao ,sasa hivi hali ni tofauti wamekuwa wakikata majani waliyootesha wenyewe na kustawi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maene hayo ,na sasa hawaingii tena katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro kukata majani.
Majani kwa ajili ya mifugo kwa sasa yanapatikana na hata afya sasa imeanza kurejea tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mmoja wa wafugaji Ludovick Meela Serik akifurahia hali ya upatikanaji wa majani kwa ajili ya mifugo yake ilivyo sasa.
Kina mama ambao wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha Mboga mboga wamekuwa wakifanya biashara vizuri kutokana na upatikanaji wa mboga ambazo kwa sasa zimekuwa zikipatikana kwa wingi tofauti na hapo awali ambapo wamekuwa wakisafirisha mboga hizo hadi nchi jirani ya Kenya.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la FLORESTA Bw. Richard Mhina akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) namna ambavyo shirika lake lilivyo saidia vikundi mbalimbali katika kampeni za utunzaji Mazngira kwa kuotesha miti pamoja na uanzishwaji wa vitalu vya miti.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Dah kaka Michuzi uchokozi mwingine!! umenikumbusha kwetu...X-mass ifike haraka niende dahh nimepamiss sana

    ReplyDelete
  2. Tuendelee kuhifadhi mazingira tusikate miti ovyo, tukilazimika kukata ili tupikie au kujengea tukate mmoja tupande miti kumi, la sivyo tukiharibu vyanzo vya maji hali ya hewa itabadilika na tunaweza kuwa na sehemu zinazogeuka kuwa jangwa ambalo kilimo chake hakitawezekana.

    ReplyDelete
  3. Haya sasa ndo maendeleo ya kweli wenyewe wanasema sustainable developments kila pembe ya Tanazania hasa kule kwenye mvua nyingi tujitahidi sana kupanda miti magereza,vyuo,shule,tassis binafsi na watu binafsi panda miti kwa wingi maji yanakauka kwa speed ya kutisha sana,bila shaka kutakuwa na vita ya kugombea maji hasa vijijin muda si mrefu...Tuawaachie watoto wetu nchi ya kijani hongera sana Kilimanjaro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...