Henry Kapinga, mmiliki wa KAPINGAZ Blog

Leo tarehe 08/12 ndio siku ambayo ukurasa wa historia ya maisha yangu ulifunguliwa rasmi, ni siku ambayo nilizaliwa, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniweka mpaka leo na vilevile kuwashukuru wazazi wangu kwa kunilea katika maisha yangu ya utotoni mpaka nilipoanza kujitegemea. 

Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wameshiriki kunisapoti kwa mambo mbalimbali ili mradi nifikie pale ambapo waliamini ni sehemu bora zaidi katika maisha yangu, vilevile napenda kumpongeza Mama yangu mdogo Mama Kasulus Kapinga ambaye na yeye tumezaliwa tarehe moja na mimi, nasema Hongera sana.

Ntakuwa mnyimi wa fadhila bila kuwashukuru MABLOGGER wenzangu kwa ushirikiano tulionao katika kuiendeleza tasnia hii ambayo kwetu Tanzania bado ni changa.

Namwomba mwenyezi Mungu anizidishie maisha marefu ili niweze kulitumikia Taifa langu na familia yangu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...