Balozi wa Ujerumani nchini Mh. Egon Kochanke (kushoto) akizungumza na wageni waalikwa wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kwenye hafla maalum ya kuwakaribisha na kuwapongeza wanajeshi wa kikosi cha wanamaji wa meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck, inayofanya doria katika ukanda wa Bahari ya Hindi kama sehemu ya jeshi la kimataifa linaloendesha operesheni Atalanta chini ya kamanda Peter Christian Semrau (kulia) iliyofanyika ndani ya meli hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mh. Egon Kochanke akifanya cheers na mmoja wa makamanda wa jeshi la wanamaji kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika ndani ya meli ya kivita ya Ujerumani FGS Lübeck inayofanya doria ya kubaini maharamia kwenye pwani ya ukanda wa Bahari ya Hindi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...