ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia leonyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam. 
Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika. 
Akizunumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
“Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo  ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta” alisema Luizer. 
 Aliongeza kwa kusema: "Hapa natetemeka siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki. 
 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.
 Msiba uko Kigamboni maeneo ya Mikadi Beach .
Aliyekuwa mnengua hodari wa African Stars band "Twanga Pepeta" na Extra Bongo Aisha madinda enzi za uhai wake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kweli vizuri havidumu, pumzika kwa ametutangulia tu nasi tunakuja.

    ReplyDelete
  2. Innalillahi Wainnailaihirojiun

    Mwenyezi Mungu ampuzishe mahala pema peponi.
    wadau
    FFU-Ughaibuni

    ReplyDelete
  3. Pole kwa wapenzi wa dansi na watanzania wrote kwa ujumla.pumzika kwa a man I.umemaliza kazi yako ya duniani.Elizabeth edward

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...