Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (kulia), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. 
Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers).  Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar, Othman Maulid "Mapara".
 Katibu Msaidizi wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha (kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati,  Henry Mdimu.
 Mwenyekiti wa Muda wa Jumuiya ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim Mushi (wa pili kushoto), wakati akifungua majadiliano kwa wajumbe wa kamati ya muda ya Jumuiya ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam leo. Majadiliano hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa hatua za usajili wa Jumuiya ya  Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha,  Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Lounge, jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...