Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia ) Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba , Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Serikali ya Mapunduzi ya Zanzibar, Dk. Juma Akir (kushoto) Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafii wa Anga Tanzania(TCCA) ambaye pia ni Msaidizi wa Rais wa Mambo ya Kanda, Dk. Nyamajeje Weggoro, wakishirikiana kukata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la TCAA. Uzinduzi huo ulikua sehemu ya maadhimisho ya Siku yaKimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD)
Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe, akizindua jengo la Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA). Uzinduzi huo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD). Anayeshuhudia kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu TCAA, Bw. Charles Chacha.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Charles Chacha(Kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Uchukuzi, Mh. Dk. Harrison Mwakyembe wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani(ICAD) yaliyofanyika kwenye viwanja vya TCAA. Katiti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Peter Serukamba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...