Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed (kulia)akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Simon Mwalugu kwa kutumia kifaa maalum wakati wa upimaji madereva ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unaohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja.Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya yaendayo mikoani katika mwendelezo wa kampeni hiyo inayofanyika nchi nzima na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Mbeya Mapunda Ahmed (kulia)akihakiki leseni ya dereva wa mabasi yaendayo mikoani Simon Mwalugu(kushoto)wakati wa zoezi la kupima kiwango cha pombe mwilini kwa madereva wa mabasi ya kwenda mikoani, kwa kutumia kifaa maalum ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya”Wait to Send” unayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.Katikati ni Mkuu wa Vodacom Tanzania kanda ya Nyanda za juu kusini Macfadyne Minja.Zoezi hili lilifanyika leo katika kituo kikuu cha mabasi mkoani Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ulevi si tatizo kubwa kama ujambazi wa kuteka magari.
    Maaskaru are aware of. Kila tukio huwa walijua in advance.

    Tanzania tusidanganyane hapa. Tunaumizana tu. Baada ya kukamata majambazi kutoka nchi jirani mara moja tu na waTZ wakajipenyeza humo humo...

    Jamani wa TZ tunaumizana sana....

    ReplyDelete
  2. ULEVI SIO ISSUE, ISSUE NI MWENDO KASI, JAMANI NYIE TRAFIC FANYENI UTARATIBU WA KUSAFIRI NA MABASI, HASA YANAYOKWENDA MBALI KAMA MWANZA, MBEYA JAMANI JAMANI, MWENDO WAO NI HATARI, KIASI KWAMBA BASI LIKIPATA HITILAFU HAPONI MTU. JARIBUNI MUONE, WAKIFIKA KARIBU AMBAPO WANAJUA KUNA TRAFIC WANAPUNGUZA MWENDO, WAKIVUKA TU MWENDAO HUO WA AJABU, NA WAKATI HUO ABIRIA WOTE WAMENYAMAZA KIMYA HAKUNA ANAEMWAMBIA ABIRIA PUNGUZA MWENDO, KWA KWELI MIMI NI MMOJA AMBAYE NIKISAFIRI NA BASI LINALOKIMBIA SANA HUWA NAPIGA KELELE SANA KWA DEREVA, APUNGUZE MWENDO, MAANA MIMI NI MUOGA SANA, IMENIBIDI SIKU HIZI NIKIENDA MWANZA NIPANDE NDEGE, MAANA NI AFADHALI KULIKO KUWEKA ROHO JUU. MWENDO KASI NDIO HASA CHANZO CHA AJALI JAMANI, FANYENI UTARATIBU WA KUSAFIRI NA MABASI MUANGALIE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...