Kamati ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale
Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe
yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania 2014, Carolyne
Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole chake cha mguu. Ripoti ya daktari imeonyesha kuwa
kupona kwake kutachukua mwezi mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada
ya siku kumi kuanzia sasa. Isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu virefu
(High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na tatizo lake.
Hivyo kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili na aliwakilisha Tanzania
katika mashindano ya Miss Earth ndiye atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala yake kama
mkataba unavyoainisha na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania 2014.
Kamati inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea kuwa nae bega kwa bega
katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya mkataba wa Miss Universe Tanzania kwa
mwaka mzima.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31 mwezi wa Kumi na
yalidhaminiwa na Insignia, Golden Tulip, Compass Communications, AzH Photography, Adams
Digicom, Opulence, Seif Kabelele Blog , Missie Popular blog, Urban Rose Hotel, na New York
Film Academy.
You need to fire your makeup artist
ReplyDelete