Asalaam Aleykum Ankali, Pole na majukumu. 
 Ningeomba uupatie uzi huu nafasi ili nasi tupate sehemu ya kupazia sauti kuhusu hii kero tunayopata watumiaji wa Mbozi Road, Chang'ombe, hapa Dar es salaam. 
Hili tatizo sasa limekuwa ni la muda mrefu panyeshe mvua ama isinyesha huwa pamejaa maji hivyo hivyo. tunaomba mamlaka husika (Manispaa ya Temeke) watusaidie au kwa lugha nyingine watimize wajibu wao tuondokane na hii adha.
Dimbwi lisilokauka barabara ya Mzozi Chang'ombe jijini Dar es salaam
Kupita hapa ni mshikemshike...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Duuh afadhali ankali umeweka hii, hivi ile tumw ya mazingira iko wapi? inasemekana maji haya yanatoka Kiwanda cha KIOO Ltd.

    ReplyDelete
  2. Escrow......who care!

    ReplyDelete
  3. nimekwama hapa last week, niliokolewa na vijana ambao ilibidi niwatoe kwa kidogo dogo. Haya maji sio salama hata kidogo yanawasha mno. Hii nchi mazee ni taaaabu, kodi twalipa lkn hakuna kinachofanyika.

    ReplyDelete
  4. Huwa najiuliza hivi kodi zetu zinaenda wapi?!! maana hili eneo na ofisi za manispaa zilipo hakuna hata umbali wa mita 400 lkn wanashindwa kutatua vitu km hi!! Shame!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. That is the truth, where is the money, people are paying taxes.

      Delete
  5. Kamvua kidogo tu cha leo pamegeuka bahari hakupitiki kabisa

    ReplyDelete
  6. Nilikuwa napita hii njia lkn toka gari yangu ilipowahi kukwama hapo sijathubutu tena kutumia hiyo njia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...