Kiungo Mbrazil Emerson De Olivera Neves Roque pichani kushoto akisaini mkataba leo jijini Dar,wa kutumikia Klabu ya Young Africans,Kulia ni Afisa Habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto.


Dar es Salaam. Wakati Yanga ikimpa mkataba wa mwaka mmoja kiungo Emerson De Oliveira, watani zao Simba wamemtema rasmi mshambuliaji Paul Kiongera.

Emerson amesaini mkataba huo baada ya benchi la ufundi chini ya Mbrazil Marcio Maximo kuridhika na kiwango chake na sasa ataitumikia timu hiyo ya Jangwani.

Emerson aliyekua akichezea katika timu ya Bonsucesso iliyopo daraja la pili kwenye jimbo la Rio de Janeiro anachukua nafasi ya mshambuliaji Geilson Santos "Jaja" ambaye klabu hiyo imeamua kuachana naye baada ya kutoridhishwa na kiwango chake.

Ofisa habari wa Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa Maximo ameridhishwa na uwezo na kiungo mkabaji Emerson na kusema ataisaidia timu katika michuano mbali mbali ya Ligi na Kimataifa.

Ujio wa Emerson unafanya klabu ya Yanga  kufikisha jumla ya wachezaji watano wa kimataifa, wengine wakiwa ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima, Hamis Kizza na Andrey Coutinho.

Katika hatua nyingine, klabu ya Simba imeachana rasmi na mshambuliaji Paul Kiongera anayesumbuliwa na majeruhi kwa muda mrefu na tayari mchezaji huyo ameshakubaliana na Simba kuhusu maamuzi hayo.

Habari za uhakika ambazo Globu ya jamii imezipata zinasema kuwa Kiongera huenda akaondoka nchini leo kwenda India kwa matibabu ya goti yanayomsumbua kwa muda mrefu.

Simba imelazimika kumuacha Kiongera baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na mshambuliaji Mganda, Danny Sserunkuma aliyekuwa akiichezea Gor Mahia ya Kenya.

"Ni kweli hatutakuwa na Kiongera, anatakiwa kupumzika baada ya matibabu. Hivyo lazima tuitumie nafasi yake," kilisema chanzo hicho.

Mshambuliaji huyo raia wa Uganda aliumia katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.

Mwananchi ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' kuhusiana na suala hilo hakukubali wala kukataa na kusema "Tutatoa taarifa rasmi."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...