Nianze kuliandikia hili kwa kuonyesha furaha yangu kuwa huwenda sasa kumekua na uelewa juu ya maswala ya usalama mitandao. Nalisema hili kutokana na uhalisia kwamba Jana nilipata maswali kutoka kwa watu wengi sana huku nikipata jumbe nyingi zilizofanana zikielezea juu ya tukio la benk ya NBC kuingiliwa na wadukuzi.
Wengi walinitaka pia nielezee huku nikiulizwa mbona hakuna nilichozungumza. Nilifarijika sana kwani muda uliopita wengi hawakua wakihoji juu ya maswala ya udukuzi pamoja na usalama mitandao na huwenda hii ilitokana na kutokua na uelewa wa maswala husika.
NINI HASA KILITOKEA?
Kwanza kabisa Kulikua na Itlafu ya Umeme ambayo ilisababisha baadhi ya Mashine kuzima.
Pili, Kulitokea Tahadhari ya Moto iliyosababisha wafanyakazi kuchuukua tahadhari ya kutoka nje.
Na Tatu, Mifumo ya Mobile banking (Inayotoa huduma za miamala kupitia simu za kiganjani) kushindwa kufanya kazi yake ipasavyo iliyo sababisha kutoa kiwango kisicho sawa kwa waliokua wakiangalia salio.
Matukio haya matatu yaliunganishwa na kutengeneza taarifa moja iliyo sambazwa kua kuna mdukuzi aliingilia banki ya NBC na kusababisha mifumo kutofanya kazi na hatimae kuhamisha kiasi kikubwa cha pesa. Kitu ambapo kilipelekea wafanya kazi kutoka nje ili uchunguzi zaidi uweze kufanywa.
Na anaepata taarifa anapo angalia salio anaona kunatatizo katika kiasi chake na kuamini jumbe ile. Panapotoka ufafanuzi wa taarifa hii wengi bado wanahoji bado kuna shaka niendelee kutoa ufafanuzi nini hasa kinaweza kikawa kimesababisha?
Asante kwa maelezo mazuri. Maoni yangu yanaghusia usalaama wa akaunti kwa ujumla. Pamoja na kwamba uememe ulikatika, na pia kulitokea na emergency iliyosababisha wafanyakazi watoke nje ya eneo.....swala linakuwa. Security kwenye computer network ina nguvu ya kutosha, maana hii ni nafasi nzuri kwa mtu anaejua kuiba kufanya hivyo, nadhani hili ni duku moja la wateja wa hiyo benki.
ReplyDeleteMbali na hayo benki zinatakiwa kuwa na backup ya backup ya backup ya mtandao wa ndani, na pia generator ilikuhakikisha maswala ya usalama wa hela upo na pia watu wanaofanya shughuli za benki kupitia simu na computer wanendelea kuona salio sahihi na kadhalika.
Na kama kila kitu kimepangwa sawa sawa na utaratibu wa kuhakikisha hela na salio zinapatikana vizuri hamna mtu atakuwa na wasiwasi.
Naona kama salio halikuwa sawa na kuonyesha upungufu fulani kila mtu lazima afuatilie imepungua wakati gani na kwa kiasi gani. Benki nayo lazima ichunguze upungufu wa hela kama ni akaunti mbili tatu ama akaunti 50,500, 1000 au mkupuo wa account. Kama ni mkupo wa akaunti, basi uwizi umetokea.
Hivyo wateja wengine wanafahamu mambo kama haya hutokea ndiyo maana roho za watu zipo juu.
Sijui benki itaweza vipi kutoa utaratibu wakuhakikishia wateja kuwa akaunti zao zipo sawa.